The House of Favourite Newspapers

Yaliyojiri Lowassa Aliporipoti kwa DCI Kuhojiwa

0
Edward Lowassa

 

Nusu saa baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwasili katika ofisi ya mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, kama alivyotakiwa kufanya Juni 29, ameruhusiwa na kutakiwa kurudi tena Alhamisi ijayo.

 Mwanasheria wa Lowassa, Peter Kibatala amezungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa Lowassa ametakiwa kurudi Alhamisi bila sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo kuwekwa wazi.

“Hatujaambiwa kwa nini ila tumeambiwa tuje alhamisi ijayo kwa ajili ya maelekezo na kuwasikiliza zaidi,” alisema

Hii ni mara ya tatu kwa Lowassa kwenda katika ofisi za DCI ambako anahojiwa kwa tuhuma za uchochezi.

 Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alihojiwa Juni 28 na Juni 29 na Wakili Kibatala alizungumza na wanahabari mara baada ya mahojiano hayo.

Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya kichochezi Juni 23, mwaka huu katika futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

 

Leave A Reply