The House of Favourite Newspapers

Yanga hii weka mbali na watoto Yanga

0


YANGA imetoa zawadi nzuri ya Krismasi kwa mashabiki wake baada ya kutoka nyuma na kuifunga Biashara United mabao 2-1 katika mchezo mkali wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, jana Jumapili siku ya Boxing Day.

Biashara ilianza mchezo huo kwa kasi na kuwashtua Yanga kwa bao la mapema la dakika ya 2 lililofungwa na Atupele Green baada ya kipa wa timu ya taifa ya Mali, Diarra Djigui kuutema mpira uliomkuta mfungaji ambaye hakufanya kosa.

Dakika ya 39, Fiston Mayele alisawazisha kwa bao safi la kideoni kwa mtindo wa acrobatic (yaani kuruka kwa kujibinua kinyumenyume na kufunga bao kali), akitumia vizuri pasi murua ya Mcongoman, Shaban Djuma.

 

Katika mchezo huo wa jana, kiungo mpya wa Yanga, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ alikuwa jukwaani akifuatilia mchezo huo akiwa amekaa na baadhi ya viongozi wa Jangwani.

Yanga walipata bao la ushindi dakika ya 79 likifungwa na Said Ntibazonkiza kwa penalti, na kuamsha furaha kwa mashabiki wa Jangwani. Penalti hiyo ilitokana na Jesus Moloco kuchezewa faulo ndani ya 18.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga iwe na uhakika wa kumaliza mwaka ikiwa kileleni, ikiwa na pointi 26 baada ya kucheza michezo 10. Kwa upande wa Biashara, wanaendelea kusaka ushindi wao wa pili wa ligi msimu huu, wakibaki na pointi nane katika nafasi ya 14.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply