The House of Favourite Newspapers

Ruvu Nao Wataka kujipigia KMC

0

TIMU ya Ruvu Shooting ya Pwani imetamba kuishushia kipigo kikali wapinzani wao KMC watakayokutana nayo kesho Jumanne katika mechi ya Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

 

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa inyeshe mvua au liwake jua ni lazima waibuke na pointi tatu za mchezo huo kwa kuwa wamechoka kufungwa lakini pia wanahitaji pointi hizo ili waweze kukaa katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

 

“Hata kama itatokea hali gani ya hewa pale uwanjani yaani iwe jua ama mvua ni lazima tuifunge KMC na kupata pointi tatu zitakazotuweka sehemu nzuri katika msimamo wa ligi hii,” alisema Bwire.

ABDALLAH ZALALA PWANI

Leave A Reply