The House of Favourite Newspapers

Yanga Kutangaza Ubingwa Leo

0

Na: Omary Mdose | CHAMPIONI| Dar es Salaam

HATIMAYE Simba wamekubali kwamba kama wakifungwa leo, basi Yanga bingwa.

Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, amesema wapo tayari kwa mchezo wao wa leo Ijumaa dhidi ya Stand United, lakini akatoa angalizo kwa vijana wake akihofia Yanga  kuchukua ubingwa mapema.

Simba ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 62, leo Ijumaa itapambana na Stand United kwenye mchezo wa ligi hiyo utakaopigwa katika  Uwanja wa Taifa, Dar.

Ligi hiyo kwa sasa inaongozwa na Yanga yenye pointi 62 kama Simba, lakini ina mabao mengi ya kufunga huku ikifungwa machache hali inayowafanya wawe juu.

Simba ikicheza leo, itabakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Mwadui, huku Yanga ikiwa nayo mitatu ambapo mmoja itacheza kesho dhidi ya Mbeya City, kisha Jumanne ijayo itapambana na Toto Africans kabla ya kumalizana na Mbao FC, Jumamosi ya mwisho ya mwezi huu.

Mayanja amesema: “Tunaendelea kupambana kuhakikisha tunashinda michezo yetu yote iliyobaki, lakini tunaangalia na wapinzani wetu nao wanafanyaje.

“Tunafahamu kwamba tukiteleza katika mchezo huu tunaweza kuukosa ubingwa na kuchukuliwa na Yanga mapema kabla ligi haijamalizika, hatutaki hali hiyo itokee, hivyo vijana  wangu ni lazima wapambane kuzisaka hizi pointi.”

LIVE: Salum Mkemi Amfungukia Ngoma, Yanga Kukosa Uwanja wa Mazoezi

Leave A Reply