The House of Favourite Newspapers

Mtoto Atibua Fungate ya Koleta

0

NA HAMIDA HASSAN | IJUMAA | STAR MIX

FUNGATE ya mwigizaji wa kitambo Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ aliyokwenda kuifanyia Bagamoyo baada ya kufunga ndoa juzikati, imetibuliwa na mwanaye mchanga kwa sababu ilibidi aongozane naye kwa kuwa ndiyo kwanza ana umri wa miezi miwili.

Akizungumza na Ijumaa, Koleta alisema kuwa, hakuwa na namna nyingine zaidi ya kwenda na mtoto wake kwani ni mdogo na isingewezekana kumuacha, jambo ambalo limemfanya asiifurahie fungate hiyo.

“Hivi ninavyoongea tunajipanga kurudi Dar kutoka Bagamoyo kwa sababu fungate yenyewe haikuwa na raha, si unajua mara mtoto analia hivyo inabidi umuangalie, yaani imekuwa ya tofauti na maharusi wengine,” alisema Koleta.

Leave A Reply