The House of Favourite Newspapers

Yanga SC Kurudi Dar Leo Usiku

0

LEO Jumatano Yanga watakuwa na dakika 90 za kupambana na Kagera Sugar kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara lakini baada ya mechi hiyo fasta tu watageuza kurudi Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa kupambana na Simba.

 

Mabosi wa Yanga ndiyo ambao wameamua suala hilo kwa ajili ya timu hiyo kutopoteza muda wowote ule baada ya kumalizana na Kagera kutokana na uzito wa mechi na Simba ya nusu fainali.

 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli ameliambia Championi Jumatano, kuwa kikosi hicho kitarudi Dar haraka baada ya kupambana na Kagera kutokana na muda mdogo wa kujiandaa na mechi yao na Simba.

“Plani zilizopo ni kuwa baada ya mechi na Kagera Sugar tu hatutakuwa na muda wowote tena wa kuendelea kubakia mkoani humo badala yake tutageuka na kurudi Dar usiku.

 

“Tunafanya hivyo kwa sababu hakuna muda wa kujiandaa zaidi wakati tukielekea kwenye mechi yetu na Simba. Tunataka kurudi Dar mapema tuanze maandalizi ya mechi hiyo na wala timu haitaenda kokote kujiandaa,” alimaliza Bumbuli.

 

Eymael ataka kulipa kisasiKwa upande mwingine Kocha wa Yanga, Luc Eymael amekumbushia juu ya mechi na Kagera kwa kusema kwamba anataka kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-0 na timu hiyo.

 

“Wakati nakuja Yanga, Kagera Sugar ndiyo timu ya kwanza kunifunga kwa hiyo ni lazima nilipize kisasi kwao wakati huu ambao ninakutana nao. Nikimalizana na Kagera na kuhakikisha tunashinda ndiyo nitageukia kufikiria mechi yetu ya nusu fainali na Simba.”

Stori: Said Ally,Dar es Salaam

Leave A Reply