WAKATI timu za Yanga na Simba zikitarajiwa kuvaana Jumamosi, Oktoba 28, mwaka huu, macho ya mashabiki wengi wa soka wa klabu hizi kubwa yapo kwa baadhi ya nyota kadhaa ambao wameonekana mwiba hasa katika michezo hiyo saba ya mzunguk o wa kwanza a m b a y o t a y a r i i m echezwa.
Simba na Yanga zimecheza michezo saba na zina alama 15 kila mmoja huku zikitofautiana katika mabao ya kufunga na kufungwa na zikiendelea kuchuana kwa hali ya juu licha ya ligi kuonekana kuwa bado mbichi.
Wafuatao ni kati ya wachezaji ambao wameweza kuonyesha uwezo wa hali juu katika michezo iliyopita na kwenye pambano baina ya vikosi hivi viwili Jumamosi hii wana kazi kubwa ya kuchungwa, lakini pia ndiyo watakuwa nyota ambao watafuatiliwa kwa ukaribu na mashabiki.
IBRAHIM AJIBU – YANGA
Amekuwa mwiba kwa sasa kutokana na uwezo anaouonyesha hasa kwa upande wa upachikaji mabao ambapo tayari katika michezo saba ya Yanga amefunga mabao matano na kuifanya timu hiyo kuwa sawa kwa pointi 15 na Simba.
Kwa mabeki wa Simba wanatakiwa kuwa macho kwa sababu ana uwezo mkubwa wa kubadilisha matokeo hasa kwenye mambo aliyoyafanya kwenye mechi mechi na Njombe Mji na Stand United. Msimu uliopita alikuwa Simba.
EMMANUEL OKWI-SIMBA
Kwa sasa straika huyu Mganda amebatizwa jina la mwanaume wa Dar kutokana na mabao yake yote nane kufunga jijini Dar.
Kasi na uwezo wa kufunga unamfanya naye achungwe na wapinzani kwani tangu arejee katika kikosi hicho ambacho aliacha n a nayo msimu wa 2014/15, mpaka sasa ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara.
OBREY CHRIWA- YANGA
Mzambia huyo ni mmoja kati ya washambuliaji ambao wamekuwa tegemezi kwa Yanga msimu huu ingawa bado kuna w a c h e zaji wageni kwenye nafasi a n a y o c h e z a kama Amissi T a m b w e r a i a w a B u rund i n a Mzi m b a b w e , Donald Ngoma ambao msimu huu wamekumbwa na majeraha tofauti na msimu uliopita, naye kama Ajibu ni moto wa kuotea mbali kwa sababu ya uwezo anaouonyesha.
SHIZA KICHUYA-SIMBA
Tangu atue k a t i k a k i k o s i c h a S imb a m s i m u uliopita amekuwa ni mmoja kati ya wachezaji ambao wana rekodi ya kuifunga Yanga. Msimu uliopita mchezo wa awali waliotoka sare ya 1-1 ndiye alifunga bao hilo na mzunguko wa pili Simba ilishinda mabao 2-1 na alifunga bao moja, ni wazi ni mmoja kati ya wachezaji ambao wamekuwa wakiinyima usingizi timu ya Yanga msimu huu.
HARUNA NIYONZIMA- SIMBA
Katika mchezo wa Jumamosi kiungo huyu matata ni lazima atataka kuonyesha makali yake kwa wapinzani hao ambao msimu uliopita alikuwa akiwatumikia kwa kiwango cha hali ya juu. Niyonzima anatazamiwa kutazamwa kwa jicho la kitofauti kwa sababu kwanza anakutana na timu yake ya zamani hivyo watataka kuona nini anakifanya ukizingatia hana kiwango kizuri tangu atue Simba.
PIUS BUSWITA – YANGA
Kiungo huyu ni wazi hasira zake huenda zikaishia kwa Simba baada ya kukosa mechi kadhaa za awali kutokana na kuwa na utata kwenye usajili wake na mechi ambazo amecheza hivi karibu ameonyesha kiwango cha hali juu na ameifungia bao moja pekee.
MAKALA: MARTHA MBOMA | CHAMPIONI JUMATANO