The House of Favourite Newspapers

YANGA WAIBIPU SIMBA SC

MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussein Niyika amesema endapo timu hiyo itaibuka na ushindi dhidi ya Township Rollers ya Bot­swana, basi Simba ijiandae ku­kumbana na kipigo kikali kwe­nye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Nyika alisema: “Tupo Botswana hivi sasa tukiendelea na mikakati yetu ya kuhakikisha tunawafunga Township Rollers lakini pia tunajiandaa na mechi yetu na Simba ambayo tutaku­tana nayo hivi karibuni.

 

“Hata hivyo, endapo tutashin­da mechi hiyo ya kesho basi Sim­ba wajiandae kwa kipigo kwani tutakuja kwa nguvu mpya katika mechi hiyo ya ligi kuu.

“Nasema hivyo kwa sababu vijana wetu wana ari lakini pia nguvu mpya ya kupambana to­fauti na awali.”

Sweetbert  Lukonge, Dar es Salaam.

Comments are closed.