The House of Favourite Newspapers

Yanga Watinga Nusu Fainali FA, Yaipiga Alliance Kirumba

KLAUS Kindoki leo amekuwa shujaa wa Yanga baada ya kuokoa penalti ya mwisho iliyopigwa na nahodha wa timu ya Alliance FC, Siraj Juma.

 

Dakika 90 za mchezo wa leo wa hatua ya fainali ulikamilika kwa Alliance kutoshana nguvu na Yanga kwa kufungana bao 1-1.

 

Yanga walitangulia kufunga bao dakika ya 38 lililofungwa na Heritier Makambo na kwa upande wa Alliance bao lilifungwa na Johson James.

Klaus Kindoki

Baada ya mwamuzi kuamua matuta, Yanga walianza kupiga kupitia beki kisiki Kelvin Yondani ambaye aligongesha kwenye mwamba, Paul Godfery alifunga penalti yake,Thaban Kamusoko alifunga kwa staili ya paneka, Mrisho Ngassa penalti yake iligonga mwamba na Haruna Moshi alifunga penalti kiufundi.

 

Kwa upande wa Alliance penalti ya kwanza ilifungwa na Joseph John, Martin Kigi aligongesha kwenye mwamba, Dickson Ambundo alikosa penalti yake, Jofrey Luseke na Samir Vicent alifunga penalti.

 

Baada ya kumaliza penalti 5 za awali kwa timu zote matokeo yalisoma 3-3 baada ya Yanga kukosa penalti 2 na Alliance pia kukosa penalti mbili.

 

Hatua ya kupiga penalti moja moja Deus Kaseke alishinda penalti yake na kwa upande wa Alliance nahodha Siraj Juma shuti lake liliokolewa na Kindoki.

 

Kwa ushindi huo, Yanga wanatinga hatua ya nusu fainali na kuifuata Lipuli ya Matola.

HABARI NA LUNYAMADZO MYUKA | GPL

Comments are closed.