The House of Favourite Newspapers

Yanga yafuata majembe matatu

BAADA ya kumwagiwa mamilioni ya usajili wa awali, Kocha Mkuu wa Yanga, raia wa DR Congo, Mwinyi Zahera, hatimaye amefanikiwa kumalizana na wachezaji watatu wa kimataifa kwa kuwapa mikataba ya awali.

 

Ijumaa iliyopita, Zahera alikabidhiwa zaidi ya milioni 80 na kamati maalum ya hamasa ya timu hiyo kwa ajili ya kwenda kuingia mikataba ya awali na wachezaji wawili, mmoja raia wa Ivory Coast na Mnyarwanda anayechezea ligi ya Kenya, lakini mbali na hivyo pia amefanikiwa kumsainisha mkataba wa awali mchezaji mwingine kutoka DR Congo.

 

Chanzo makini kimelieleza Championi Jumatano kuwa, Zahera atamaliza usajili wake wa kimataifa mapema kwa kuwa kati ya wachezaji wote aliokuwa akiwahitaji ameshaanza kumalizana nao kwa kuwapa mkataba wa awali na kwamba anashindwa kuwaweka wazi kwa kuhofi a kuingiliwa usajili wake na timu zenye uwezo mkubwa.

 

“Kamati ya hamasa ya uchangiaji tayari imeshaanza kutekeleza majukumu yake kwa kocha kwa kumpatia kiasi cha awali alichoomba na kwamba wamemtaka aseme mapema pale anapomalizana na mchezaji ili na waweze kukusanya michango kwa malengo kwani mbali na kumtafutia fedha za usajili, pia wana jukumu la kukusanya fedha za kulipa mishahara ya wachezaji hao,”kilisema chanzo hicho.

Musa Mateja.

SPOTI HAUSI: Sababu Zilizowatoa SERENGETI BOYS Kwenye AFCON!

Comments are closed.