The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaipiga Mtibwa Sugar Bao 1-0, Molinga Atupia

0

Bao pekee la mshambuliaji David Molinga limetosha kuipa Yanga ushindi 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

Molinga alifunga bao hilo pekee katika dakika 50, akiunganisha vizuri krosi ya Ditram Nchimbi na kuihakikishia Yanga pointi tatu na kupanda hadi nafasi tatu ikiwa pointi 31, wakiwa nyuma kwa pointi 13 kwa vinara Simba (44) huku Azam nafasi ya pili (37).

 

Bao hilo linamfanya Molinga kufikisha mabao 6 katika orodha ya wafungaji bora inayoongozwa na Meddie Kagere wa Simba (12).

 

Kiwango bora alichoonyesha Molinga kiliwafanya mashabiki wa Yanga kumshangilia kwa nguvu wakati anatolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Yipke Gilman.

Leave A Reply