The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaitungua 3-2 JKT Tanzania

YANGA leo imeibuka na pointi tatu muhimu mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Uhuru.

 

David Molinga ndiye aliyefunga bao lake la ushindi leo uwanja wa Uhuru kwa mpira wa adhabu uliozama jumla ndani ya lango.

Huu ni mchezo wa sita kwa Yanga na mchezo wa pili kwa kaimu kocha mkuu Boniface Mkwasa kuongoza na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

 

Ngoma ilianza kuwa ngumu kwa JKT Tanzania kipindi cha kwanza baada ya Yanga kuandika bao la kwanza kupitia kwa Patrick Sibomana dakika ya 11 na ilisawazishwa dakika ya 13 na Adam Adam dakika ya 13.

Mambo yalizidi kuwa magumu kwa JKT Tanzania baada ya bao la pili kupachikwa dakika ya 22 na Juma Balinya kabla ya David Molinga kufunga bao la tatu kwa mpira uliokufa kwa JKT Tanzania dakika ya 35 na Danny Lyanga alifunga bao la pili dakika ya 45.

 

Kipindi cha pili timu zote zilicheza ka hesabu kali na hakuna timu iliyoona lango la mwenzao na kuifanya Yanga kuibuka na ushindi wa jumla ya pointi tatu mazima mbele ya JKT Tanzania. Aliyeibeba Yanga leo ni Deus Kaseke ambaye alitoa pasi zote za mabao kwa Balinya na Sibomana.

Comments are closed.