The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaitungua Azam Bao 1-0

Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar. Bao pekee la Yanga limefungwa na mchezaji Mrisho Ngassa dakika ya 13 ya mchezo huo baada ya kumalizia pasi ya Ibrahim Ajibu.

 

Katika mechi hiyo iliyokuwa mhimu kwa kila timu, ilikuwa na mvuto na upinzani wa aina yake kutokana na timu zot hizo kubwa kuwa nafasi tatu za juu na kila mmoja akiitaka nafasi ya kwanza kuelekea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.

 

Yanga wameendelea kubaki kileleni akifikisha pointi 77 na michezo 33, huku Azam akibaki nafasi ya tatu na pointi zake 66 na michezo 33, nyuma ya Simba waliyopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 69 na michezo 27.

Comments are closed.