Yanga Yamchomoa Kiungo Stars Fasta

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utawaita wachezaji wote wa timu hiyo ambao wapo kambini kwa sasa kwenye timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia kuja kuhudhuria katika kilele cha Wiki ya Mwananchi.


Timu ya Taifa ya Tanzania
iliingia kambini Agosti 25, tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo dhidi ya DR Congo utakaofanyika Septemba 2, nchini DR Congo.

Wachezaji Yanga ambao wameenda kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania ni Feisal Salum, Dickson Job, Zawadi Mauya na Ramadhani Kabwili.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa Mkurugenzi Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro, alisema kuwa tayari imeshawasiliana na uongozi wa timu ya taifa juu ya kuwaomba wachezaji hao kwa ajili ya kuja kushiriki Siku ya Mwananchi kisha kurejea tena kambini.

“Tayari tumeshaongea na uongozi wa timu ya taifa ya Tanzania juu ya kuwaomba wachezaji wetu wote katika mchezo wa kilele cha siku ya mwananchi dhidi ya Zanaco FC na tayari ombi letu limekubaliwa.

 

“Hivyo mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi juu ya kuwakosa wachezaji hao na kilichobaki kwa sasa
mashabiki wanatakiwa wafike
kwa wingi kwani kutakuwa na mambo mengi mazuri kwa ajili yao,” alisema kiongozi huyo705
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment