Yanga Yampa Beno Masharti Mazito

Beno Kakolanya

YANGA imemtaka Beno Kakolanya kuwathibitishia kwa maandishi kwamba hatakuwa na madai yoyote endapo
wakiridhia kutengua mkataba wake. Lakini mwanasheria wa kipa huyo,Leonard Richard akawajibu fasta tu kwamba hakuna noma hawatadai hata shilingi.

 

Hadi sasa Beno amekosa mechi 12 kati ya 20 walizocheza Yanga ambapo amecheza mechi nane tu tangu msimu huu uliopoanza Agosti 2018 ambapo kocha huyo alieleza wazi kuwa mlinda mlango huyo akirudi yeye anaondoka.

 

Akizunumza na Spoti Xtra, Mwanasheria wa Beno, Richard alisema kuwa, Yanga wamemtaka Beno kuthibitisha kuwa hawatokuwa na madai kabla ya kuvunja mkataba jambo ambalo wamelitekeleza ambapo wameahidi kuwapa majibu Jumatano.

 

“Yanga wamesema kuwa watatupatia majibu ya barua yetu siku ya Jumatano kwa kuwa niliwaomba walitekeleze suala hilo kwa haraka kwa kuwa limechukua muda hivyo tunatariaji kulipata jibu la juu ya kuvunja ama wataamua nini siku ya Jumatano.

 

“Awali kabla ya kufanya chochote kuna vitu walitutaka tuvitekeleze ambavyo tayari tumeshavifanya likiwemo suala la kuthibitisha kwamba hatutakuwa na madai iwapo watavunja mkataba suala ambalo tayari tumeshalitekeleza .

 

“Hivyo baada ya hapo ndio tutajua nini cha kufanya baada ya kupata barua kutoka Yanga kwani makubaliano yangu na Beno yapo kwa ajili ya kusimamia katika suala zima la kuvunja mkataba wake,” alisema Richard.

STORI NA KHADIJA MNGWAI

Loading...

Toa comment