The House of Favourite Newspapers

Yanga Yampasua Kichwa Kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ a

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefichua kuwa, kufanya vizuri kwa Yanga katika michuano ya kimataifa, kumepelekea aongeze umakini mkubwa katika machaguo ya wachezaji anaowahitaji kwenye kikosi chake kwa lengo la kufanya makubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Robertinho ametoa kauli hiyo, huku ikiwa tayari Simba imetangaza kuachana na kiungo mshambuliaji wake, Agustine Okrah raia wa Ghana kutokana na kushindwa kufikia malengo ya timu hiyo msimu huu.

Akizungumza na Spoti Xtra, Robertinho alisema, malengo yake yapo katika kuhakikisha Simba inafanya usajili wa maana kuelekea msimu ujao ili waweze kufikia malengo makubwa kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao Yanga.

“Tupo na mechi mbili za mwisho kwenye ligi kabla ya kuanza msimu ujao kwa kufanya usajili halafu maandalizi yatafuata, kwa sababu malengo yetu bado ni makubwa baada ya kushindwa kuyafikia msimu huu, maana ukiangalia hakuna kombe lolote ambalo tumelipata.

“Nadhani kuna haja ya kuwa makini katika usajili kwa kuhakikisha napata kile ambacho ninakiomba kutokana na mahitaji ya timu kuelekea msimu mpya kuanzia ligi ya ndani na michuano ya kimataifa, kwa sababu kila mmoja ameona namna wapinzani wetu (Yanga) walivyofaidika kutokana na kuwa na kikosi kizuri,” alisema Robertinho.

Ikumbukwe kuwa, msimu huu, Yanga imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 2004, ambapo ilipoteza mbele ya USM Alger.

STORI NA IBRAHIM MUSSA

KAIMU SHEIKH wa MKOA wa DAR, SHEIKH WALID, ALHAD MUSSA WAFUNGUKA MAZITO – “SOTE ni NDUGU”…

Leave A Reply