The House of Favourite Newspapers

Yanga Yamtorosha Kiungo, Aiacha Klabu Yake Kwenye Mataa

0

Na Wilbert Molandi|CHAMPIONI|GPL
YANGA ni kama imeifanyia umafia Mbao FC baada ya kumtorosha beki mbishi wa pembeni mwenye kasi, Jamal Mwambeleko.
Mwambeleko ni miongoni mwa mabeki bora namba 3 walioonyesha viwango vizuri msimu uliopita ambaye alifanikiwa kumzuia winga wa Yanga, Simon Msuva na kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya.
Beki huyo, hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kujiunga na klabu yoyote kutokana na mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mratibu wa Mbao, Zephania Nyashi alisema kwa mujibu wa taarifa ambazo wamezipata, beki huyo amejiunga na Yanga na wakati wowote anatarajiwa kusaini mkataba Yanga.
Nyashi alisema, beki huyo juzi Jumamosi walimuita kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo ya kumuongezea mkataba pamoja na kiungo wao, Pius Busita lakini cha kushangaa hakutokea.
Aliongeza kuwa, mara baada kutotokea walifanya jitihada za kujua yupo wapi, lakini wakapata taarifa yupo kambini na Yanga akijiandaa na michuano hiyo mipya ya SportPesa Super Cup.
“Mwambeleko tunamshangaa sana kwa kitendo hiki alichokifanya, ni kama ametutoroka vile na kwenda kujiunga na Yanga.
“Kwa sababu mwishoni mwa wiki iliyopita tulimuita yeye na Busita kwa ajili ya kuzungumza nao, lakini cha kusikitisha hakutokea na badala yake akaja Busita pekee.
“Baada ya kuona hajatokea tukajua kabisa hatutakuwa naye kwenye msimu ujao kutokana na viongozi wa Yanga kumuhitaji kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu, hivyo sisi tumeachana naye.”
Alipotafutwa Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh kuhusiana na taarifa za beki huyo kuanza mazoezi alisema: “Wapo wachezaji watatu tulioanza nao mazoezi siku hizi mbili pamoja na kuingia kambini tukijiandaa na SportPesa Super Cup itakayoanza kesho (leo), hivyo tusubirie kesho (leo) mtawaona wote.

Leave A Reply