The House of Favourite Newspapers

Yanga Yatamba Kuwapiga Mvua ya Mabao Real Bamako ya Mali Kwa Mkapa

0

RAIS wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema baada ya kubanwa na wenyeji wao, Real Bamako ya Mali kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika sasa watahakikisha kwenye mchezo wa marudiano wanawapiga bao za kutosha kama zawadi kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye hutoa Sh mil 5 kwa kila bao kwa Simba na Yanga kwenye michuano ya kimataifa.

Yanga ambayo iko nafasi ya pili kwenye kundi lao la Kombe la Shirikisho wakiwa na alama nne, walibanwa na Real Bamako ambao walisawazisha dakika za usiku na kutoka nayo sare ya bao 1-1, sasa watarudiana Machi 8, mwaka huu kwenye Dimba la Mkapa, Dar.

RAIS wa Yanga, Injinia Hersi Said.

Kikosi cha Yanga jana Jumanne kilitua nchini kikitokea Mali na tayari kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata.

Akizungumza na Championi Jumatano, Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said alisema kuwa: “Tunashukuru kupata pointi moja ugenini, haikuwa rahisi japo tulitamani kupata pointi zote tatu kutokana na uhalisia wa mchezo wenyewe.

“Ukiangalia kwa ambao tumetoka Mali tunafahamu kuwa hali ya hewa ya huko haikuwa rafiki kwetu kutokana na joto kuwa kubwa sana hivyo tuwapongeze wachezaji wetu kwa mapambano ambayo wameyaonyesha.

“Lakini pia tunashukuru kwa kukabidhiwa milioni 5 na msemaji wa serikali, Gerson Msigwa ambaye anamuwakilisha Rais wetu kipenzi, Mama Samia Suluhu Hassan.

“Hivyo nimuahidi Rais wetu kipenzi kwamba mchezo wetu ujao dhidi ya Real Bamako Machi 8 kuwa tutampa zawadi ya mabao mengi kwa Mkapa kwa kuwa ni mchezo muhimu kwetu kuweza kupata matokeo,” alisema kiongozi huyo.

Na Marco Mzumbe, Happy Laurent, Rehman Abdul, Omary Michuzi

#EXCLUSIVE: MANGUNGU ATAJA ISHU ya MASHABIKI KUMWAMBIA YANGA, SIMBA ya KIMATAIFA..

Leave A Reply