The House of Favourite Newspapers

YANGA YATOKA SARE NA KARIOBANGI SHARKS BAO 1-1

Timu ya Yanga imelazimishwa sare ya bao moja na Kariobangi Sharks katika mchezo wa kirafiki katika kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi katika mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa.

 

Katika mchezo huo Yanga ilitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini washambuliaji wake walikosa nafasi za kufunga.

 

Wenyeji Kariobangi walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Patrick Otieno dakika ya 50 baada ya walinzi wa Yanga kufanya makosa kwenye kuokoa hatari.

Goli hilo lilidumu kwa dakika saba pekee baada ya Patrick Sibomana kuisawazishia Yanga kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi mmoja wa Kariobangi kuunawa mpira ndani ya 18.

Licha ya kushindwa kupata matokeo ya ushindi lakini wachezaji wa Yanga ambao wengi wao ni wageni walicheza vizuri huku nahodha Papy Tshishimbi na Mohammed Banka wakilimiliki vizuri eneo la kiungo.

PICHA: RICHARD BUKOS| GPL

Comments are closed.