The House of Favourite Newspapers

ads

Yanga Yawaandalia dozi Ruvu Shooting Uwanja wa Mkapa Kesho Jumatatu

0

UONGOZI wa Yanga, umeweka wazi kuwa, mara baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara, sasa inafuata zamu ya Ruvu Shooting.

Yanga ambayo ilitoka kuifunga Ihefu, imesema malengo yao ni kuhakikisha wanaendelea kupata matokeo mazuri katika Ligi Kuu Bara msimu huu na kutetea ubingwa wao.

Kesho Jumatatu, Yanga wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Tulishinda mechi iliyopita dhidi ya Ihefu, sasa tunahamishia nguvu zetu kwa Ruvu Shootinga ambayo tunaamini ni timu inayohitaji sana matokeo, hivyo lazima tuwaheshimu.

“Hizi timu ambazo zinapambana katika nafasi za chini tunatakiwa kuziheshimu, kisha kupambana nazo, lakini kwa upande wetu tunajiamini na tunajua kuwa tunakwenda kufanya nini, tunakwenda kutafuta matokeo ya ushindi.

“Mashabiki wanatakiwa kuja kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kuisapoti timu yao na sisi tunawaahidi kuwapa burudani zaidi.”

STORI NA MARCO MZUMBE

MBOWE: RAIS SAMIA ALIKUA MVUMILUVU, MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI!

Leave A Reply