The House of Favourite Newspapers

Yondani atoboa siri ya kiwango chake Yanga

0

YONDANI

Beki wa kutumainiwa wa timu hiyo, Kelvin Yondani.

Hans Mloli,
Dar es Salaam
UKIACHANA na balaa wanalolifanya kina Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko pale Yanga lakini beki wa kutumainiwa wa timu hiyo, Kelvin Yondani naye ni habari nyingine kwa sasa kutokana na msaada alionao klabuni hapo.
Tangu alipoumia nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Yondani amekuwa mhimili mkubwa wa safu ya ulinzi ya timu hiyo na zaidi akichukua jukumu la kupiga mikwaju ya penalti ambayo hajafanya makosa. Amefunga zote tatu alizozipata hivi karibuni. Moja kwenye Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, nyingine Mapinduzi Cup na ile ya kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda.
Akizungumzia hali hiyo, Yondani alifunguka kuwa imetokana na ukongwe wa soka la Bongo alionao lakini pia kupunguza baadhi ya ratiba nyingi zilizokuwa zikimzonga na kugeukia soka pekee huku akipata muda wa kupumzika na kutafakari juu ya kazi yake.
“Kweli hata mimi naona kwa sasa nimekuwa nikipanda kadiri siku zinavyosogea na nashukuru Mungu kwa hilo lakini nikuhakikishie tu imekuwa hivi kwa sababu nimepunguza ratiba nyingi ambazo hazina maana, kwa hiyo napata muda pia wa kufikiri kuhusu soka, ndiyo maana nipo hivi,” alisema Yondani.
Yondani amewaongoza mabeki wengine kuhakikisha Yanga hairuhusu bao lolote katika mechi tano mfululizo za Ligi Kuu Bara walizocheza mpaka sasa.

Leave A Reply