The House of Favourite Newspapers

A-Z KILICHOMUUA BABA ALIKIBA, FAMILIA YAFUNGUKA ‘ALIKUWA DEREVA’ – VIDEO

Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba, Mzee Saleh Kiba amefariki Dunia alfajiri ya leo Januari 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu na Familia ya Alikiba ambaye amezungumza na global TV amesema mwili wa marehemu bado umehifadhiwa Muhimbili na msiba upo nyumbani kwao Kariakoo na kwamba mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni katika Makaburi ya Kisutu.

Inaelezwa kuwa, Mzee Kiba ambaye pia ni baba mzazi wa msanii Abdu Kiba na Zabibu Kiba amekua akiugua kwa muda sasa huku akiendelea kutibiwa.

Inna lillahi wainna ilayhi raji’un. Pole sana kwa familia ya Kiba.

Comments are closed.