The House of Favourite Newspapers

Zahera Aitaja Siri Ya Mafanikio Yanga SC

Mwinyi Zahera.

KOCHA Mkuu wa Yanga ambaye kwa sasa yupo zake Ufaransa, Mwinyi Zahera amesema siri kubwa ya ushindi ambao timu yake inaupata ni kutokana na timu zingine kuwadharau.

 

Yanga chini ya Zahera imekuwa na mafanikio makubwa na mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote kati ya 17 waliyocheza wameshinda 15 na sare mbili tu hivyo wana alama 47.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Zahera ambaye yuko Ufaransa ‘akisinya’(akisaini) mikataba ya biashara zake, amesema dharau wanazopata kutoka kwa wapinzani wao wamekuwa wakizitumia kama daraja la wao kupata ushindi katika michezo yao.

 

“Unajua kwamba wengi wanatuona kwamba Yanga tuna kikosi ambacho hakina wachezaji wale wenye majina makubwa hali ambayo inasababisha wakija kucheza na sisi wanatudharau kwa kuona watatufunga.

 

“Unakuta hata hizi ndogo nazo zinatudharau tena kama wakipata bao kwenye mechi ndiyo wanaondoa ile hali ya kujilinda na wanacheza kwa kushambulia wakiamini watatufunga sasa hiyo inakuwa nafasi kwetu ya kutengeneza nafasi za mabao na ndiyo hivi tunashinda tu kila mechi,” alisema Zahera ambaye ni raia wa DR Congo na Ufaransa.

Said Ally, Dar es Salaam

Comments are closed.