The House of Favourite Newspapers

Zama aibua upya machungu ya zari kwa mumewe

KUTOKANA na kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzal­ishaji wa Clouds Me­dia Group (CMG), Ruge Muta­haba ambaye ni mzazi mwenza wa Zamaradi Mketema ‘Zama’, mjasiriamali maarufu nchini Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amefunguka kuumizwa na mwanamama huyo aliyeachiwa watoto wawili wadogo.

 

Zari alionesha kutoneshwa kidonda na kukumbushwa ma­chungu na Zama kutokana na aliyekuwa baba watoto wake, Ivan Ssemwanga ambaye alifa­riki dunia na kumwachia watoto watatu.

Mwanamama Zari kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Snapchat aliandika jinsi moyo wake unavyouma na kuvuja damu kwa ajili ya Zama.

 

HISTORIA YAO INAFANANA

Akizungumza na Ijumaa Wik­ienda mtu wa karibu wa Zari alieleza kuwa Zari anaonekana kuumizwa sana na Zama kuto­kana na historia yao kufanana.

Zari alikuwa kwenye uhu­siano wa kimapenzi na Ivan ambaye walijaliwa kupata watoto watatu na baadaye wakaachana kisha akaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Muda mfupi baadaye, Ivan ambaye alikuwa akiwatunza watoto na kuwapa kila kitu, alifariki dunia.

Baada ya Ivan kufariki huku Zari akiwa kwenye uhusiano na Diamond walijaliwa kupata wa­toto wawili, lakini walimwagana na sasa kila mmoja anaendelea na maisha yake.

 

Kwa Zama nako iko hivyo­hivyo; alifanikiwa kupata watoto wawili na Ruge kisha baadaye wakaachana ambapo mwanamama huyo aliolewa na mwanaume mwingine ambaye yupo naye kwenye ndoa mpaka sasa na wamejaliwa mtoto mmoja.

 

Ruge alifariki dunia Februari 26, mwaka huu nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu na mwili wake ku­wasili nchini Ijumaa iliyopita kisha kuagwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar siku ya Jumamosi, jana ukasafirishwa kwenda Bukoba ambapo amezikwa leo.

Stori: Mwandishi Wetu, Ijumaa Wikienda

Comments are closed.