The House of Favourite Newspapers

Zantel Yashiriki Udhamini wa Shindano la ‘Shika Ndinga’ Mwananyamala

0


Washiriki wa shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha redio Efm na kudhaminiwa na Kampuni ya Zantel wakichuana katika mwendelezo wa kampeni ya Shika Ndinga iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Washiriki wawili kila mmoja alijinyakulia pikipiki yenye thamani ya Tsh1.9 milioni baada ya kuibuka na ushindi. Washiriki watano kwa upande wa wanawake na watano kwa upande wa wanaume walifuzu hatua ya mchujo.


Mmoja kati ya majaji katika shindano hilom, Said Mkumba (kushoto) akiwakagua washiriki waliokuwa wakichuana katika mwendelezo wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’.


Mmoja kati ya majaji katika shindano la Shika Ndinga (kulia), akimwonyesha kadi ya nyekundu mmoja ya washiriki katika mwendelezo wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki.


Mmoja kati ya majaji katika shindano la Shika Ndinga akimwonyesha kadi ya njano mmoja ya washiriki hao.

 

Rehema Nassoro akikabidhiwa pikipiki baada ya kuibuka kwa upande wa wanawake wakati wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’ inayoendeshwa na kituo cha redio cha Efm na udhaminiwa na kampuni ya Zantel.


Alphonse Daudi, mkazi wa Gongo la Mboto akifurahi baada ya kukabidhiwa pikipiki yenye thamani ya Sh1.9 millioni aliyoshindi kwa upande wa wanaume wakati wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’ inayoendeshwa na kituo cha redio cha Efm na udhaminiwa na kampuni ya Zantel iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Leave A Reply