The House of Favourite Newspapers

Zantel Yazindua Vifurushi vya Bure Kwa Mitandao Yote ya Kijamii

0

Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri (kulia) na Meneja wa Muziki na uendeshaji Mdundo.com, Prisna Nicholaus wakimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin (wa pili kulia) Application ya Mdundo.com ambayo wateja wa Zantel wataipata bure baada ya kujiunga na huduma mpya ya vifurushi vya bure kwenye mitandao yote ya kijamii iliyozinduliwa na Kampuni ya Zantel jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa.

Mtaalamu wa masuala ya Biashara Zantel, Rehene Cathbert Tarimu (kulia) akionyesha Application ya Mdundo.com ambayo wateja wa Zantel wataipata bure mara baada ya kujiunga na huduma mpya ya vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii iliyozinduliwa na Kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam. Katikati ni Mtaalamu wa huduma za simu Emmilina Albert Vokolawene pamoja na Mtaalamu wa masuala ya Teknolojia Zantel Salim Awadh.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akigawa Modem kwa wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM katika hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana, ambapo pia wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com bure. Anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana ambapo pia wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com bure. Kulia ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akisalimiana na Meneja wa Muziki na uendeshaji Mdundo.com, Prisna Nicholaus mara baada ya uzinduzi rasmi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam, ambapo wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki bure kupitia application ya Mdundo.com

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM katika hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii yenye lengo la kuwanufaisha hasa vijana. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa.

Leave A Reply