The House of Favourite Newspapers

Zanzibar Yajiandaa Kutoa Chanjo ya Covid-19

0

Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi amesema kwa sasa Zanzibar inaandaa utaratibu wa kuwawezesha Mahujaji kupata chanjo ya COVID-19 ili kukidhi vigezo vilivyowekwa na Serikali ya Saud Arabia mwaka huu katika kushiriki Ibada hiyo tukufu ya Hijja hatua ambayo mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaweza kuiunga mkono Zanzibar ili kufikia matakwa hayo.

Rais Mwinyi ametoa kauli hiyo jana Alhamisi, mei 20, 2021, wakati alipofanya mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), nchini Tanzania, Zlatan Milisic ambaye alifika Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha rasmi kwa Rais.

Rais Mwinyi ameeleza haja ya UN kupitia UNESCO kuuenzi Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao ni Urithi wa Dunia, kwani hivi sasa baadhi ya nyumba nyingi katika mji huo zinahitaji matengenezo kutokana na uchakavu wake.

Leave A Reply