The House of Favourite Newspapers

ZARI AMMALIZA TANASHA, KIFUA, MVUTO

Mganda Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

 

AMEMMALIZA! Ndivyo walivyoamua wafuasi wa aliyekuwa mpenzi wa Diamond (Nasibu Abdul), Mganda Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ alipowekwa kikaangoni na mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Tanasha Donna ‘Zahara Zaire’ wa Kenya. Mtifuano huu umeibuka mara baada ya Diamond kuanzisha uhusiano na Tanasha hivi karibuni na kuonesha kuwa amepagawa naye huku kila mtu akitoa maoni yake mitandaoni.

Tanasha Donna ‘Zahara Zaire’ wa Kenya.

 

MJADALA MEZANI

Mara baada ya kuona hoja mbalimbali kuhusu warembo hao, gazeti dada la hili, Ijumaa Wikienda liliuweka mjadala rasmi kupitia ukurasa wake wa Facebook na kutaka maoni ya nani ni mzuri na bora zaidi kuliko mwenzake?

IDADI YA WATU

Kwenye ukurasa huo wenye wafuasi takriban 9,373 wachangiaji waligawanyika ambapo kuna ambao walisema Zari ni mzuri na bora kuliko Tanasha, lakini wapo pia waliosema kinyume chake. Kwenye maoni hayo, upembuzi wa Ijumaa uliyachuja kwenye maeneo sita muhimu na kupata hesabu ambayo ilimbeba Zari mwenye umri mkubwa zaidi (40) kuwa juu zaidi ya Tanasha ambaye anakadiriwa kuwa na miaka 25.

 

MAENEO YA UCHUNGUZI

Maeneo hayo ambayo Ijumaa lilifanya mlinganisho kwa kufanya ‘sampo’ ya idadi ya watu 100 kwenye maeneo ya miguu, kifua, makalio, macho, mvuto wa jumla na mali au utajiri.

Zari The Boss Lady

MIGUU Katika miguu, kati ya watu 100 waliochangia, Zari alipata watu 89 ambao walisema ana miguu mizuri huku 11 wakimsifia Tanasha. Waliomsifia Zari walisema miguu yake ni mikubwa na imejengeka vizuri (miguu ya bia) tofauti na Tanasha ambaye miguu yake sio minene na ana vigimbi.

KIFUA Katika eneo hilo, licha ya Zari kuwa mama wa watoto watano, bado alimfunika Tanasha kwa kupata wafuasi 93. Baadhi ya maoni kati ya watu 93 yalieleza kuwa, kinachombeba Zari ni kutokana na jinsi matiti yake yalivyosimama na madogo tofauti na ya Tanasha ambaye yamelala na kuambulia kura 07.

KALIO Upembuzi wa Ijumaa kwenye eneo hili ulibaini kwamba, Zari alimzidi kidogo Tanasha kwani kati ya wafausi 100, 56 walisema Zari amemfunika mwenzake huyo ambaye naye alipata watu 44.

MACHO Ijumaa lilibaini, eneo hili Tanasha aliibuka kidedea kwa sababu aliweza kujikusanyia wafuasi 90 huku Zari akiambulia 10. Wengi walisema macho ya Tanasha ni mazuri na yana muonekano wa kumvutia mwanaume tofauti na Zari.

Tanasha Donna ‘Zahara Zaire’ wa Kenya.

MVUTO Katika eneo la mvuto wa jumla, wafuasi wengi walionekana kumbeba Zari kwa kusema ana mvuto zaidi kuliko Tanasha ambapo kati ya watu 100, 88 walikuwa upande wa Zari huku 12 wakimsapoti Tanasha. Waliomsapoti Zari, wengi wao walikuwa na hoja kwamba Mungu kamjalia Zari kuwa na muonekano mzuri wa asili na usiochuja kwani umri wake ni mkubwa, lakini bado analipa.

MALI AU UTAJIRI Kwenye eneo hilo, wafuasi 96 walisema Zari ana mali zaidi kuliko Tanasha ambaye anaonekana chanzo chake kikubwa cha mapato ni mshahara wa utangazaji. Maoni ya watu walioonesha kumjua Tanasha, mengi yalionesha kwamba mrembo huyo hawezi kujilinganisha kwa utajiri na Zari ambaye anamiliki vyuo na maduka nchini Afrika Kusini.

 

Walisema Zari ana magari mengi ya kifahari kulinganisha na Tanasha ambaye anatumia magari ya kawaida. Magari anayomiliki Zari ambapo Ijumaa ilishawai kuyaripoti ni kama Lamborghini Gallardo, BMW-2006, Chrysler-2008, Audi Q7-2010, Hummer H2 na Ranger Rover Sports.


UMAARUFU Kwenye eneo hilo ndiyo ilikuwa funika bovu, Zari alimuacha mbali Tanasha kwani alipata watu 99 huku mtu mmoja pekee ndiye aliyesema kuwa Tanasha ni maarufu zaidi kuliko Zari. Kwa mujibu wa maoni mengi yaliyombeba Zari yalijikita kwenye matukio makubwa ambayo Zari amekuwa akiyafanya ikiwemo ya kijamii, matamasha ya burudani kama vile Zari All White Party na mengineyo.

 

Hawakuishia hapo, walikwenda mbali zaidi kwa kusema kitendo cha Zari kumiliki vyuo kinambeba zaidi kwani amekuwa na watu wengi wanaomfahamu na kumfuatilia kutokana na matukio mbalimbali anayoyafanya. Wachache walimbeba Tanasha kwa kusema naye anaandaa matamasha kama ambavyo sasa ameshirikiana na Diamond kuandaa Wasafi Festival pande za Mombasa na Nairobi, Kenya, lakini hata hivyo walikosolewa kwa kuambiwa kuwa shoo hiyo imeandaliwa na redio anayofanya kazi mrembo huyo iitwayo NRG.

Hoja nyingine waliyoisimamia waliompa alama Zari, walisema ana wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. Zari ana wafuasi milioni 4.7 huku Tanasha akiwa na wafuasi laki mbili na arobaini.

DIAMOND APEWA MTIHANI Pamoja na maeneo hayo ambayo yanaonesha kumpa ushindi mnono Zari, wafausi hao walimpa mtihani mgumu Diamond kwa kumtaka arudi kwa Zari kama inawezekana kwa kuwa ana sifa za ziada tofauti na Tanasha.

ZARI MAMA BORA Walisema kwanza Zari ni mama bora, amemzalia watoto wawili, lakini pia ni mwanamke mpambanaji anayejua kutafuta pesa na kulea familia tofauti na Tanasha ambaye bado haijui leba inafanaje.

Comments are closed.