The House of Favourite Newspapers

ZEC Yamsimamisha Maalim Seif Kufanya Kampeni

0

TUME  ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemsimamisha mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, kutofanya mikutano ya kampeni za urais kwa siku tano baada ya kuonekana na kosa la uvunjifu wa maadili.

 

Akitangaza maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Katibu wa Kamati hiyo ya Maadili, Khamis Issa Khamis, amesema tume ilipokea malalamiko kutoka kwa mgombea wa urais wa Chama cha Demokrasia Makini, Ameir Hassan Ameir, dhidi ya mgombea Maalim Seif ya kuhamasisha wanachama wake wakapige kura siku ya kura ya awali.

 

Katibu wa kamati amesema kamati ilisikiliza hoja zote na kuona kuwa mgombea Maalim Seif ametenda kosa hilo na kumpa adhabu kwa mujibu wa sheria kifungu cha 23 D za kanuni za maadili. Kamati hiyo ya maadili imetoa fursa kwa Maalim Seif kukata rufaa endapo hataridhika na maamuzi hayo.

 

Leave A Reply