The House of Favourite Newspapers

Zimbambwe Yaichapa Taifa Stars 3-0

Taifa Stars (1)

KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo kimeshindwa kufurukuta baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa wenyeji Zimbabwe.

Katika mchezo huo wa kirafiki uliopigwa nchini Zimbabwe, Stars walianza kuruhusu bao dakika ya tisa baada beki wa Stars, Erasto Nyoni kushindwa kuuzuia mpira uliotua kwa Knowledge Musona aliyeiandikia timu yake bao la kwanza.

Mpaka mapumziko bado Zimbambwe walikuwa mbele kwa bao 1-0. Katika dakika ya 53 ya mchezo, mchezaji Rusike Mathew aliiandikia Zimbabwe bao la pili baada ya kupiga shuti kali linalojaa wavuni na kumshinda mlinda mlango wa Stars, Aishi Manula.

Zimbabwe waliendelea kucheza soka safi na katika dakika ya 56 walipata bao la tatu kupitia kwa Mushekwi.

Mpaka dakika ya 90, matokeo yalikuwa Zimbabwe 3-0 Taifa Stars.

Kwa matokeo ya leo inaonyesha kikao cha Stars bado kinahitaji maboresho makubwa ili kuweza kuleta changamoto kwa timu watakazokuwa wanakutana nazo uwanjani, hivyo kocha wake Charles Boniface Mkwasa bado ana kibarua cha kuiboresha timu ili iweze kupata matokeo mazuri.

halotel-1

Comments are closed.