The House of Favourite Newspapers

Zitto Apongeza Ushindi wa CCM Muhambwe

0

KIONGOZI wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameipongeza CCM kwa ushindi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Muhambwe.

 

Uchaguzi huo ulifanyika jana na Dk Florence Samizi wa CCM, ametangazwa mshindi kwa kupata kura 23,441 kati ya kura halali 34,656 zilizopigwa.

 

Kutokana na ushindi huo, jana Jumapili Mei 16, 2021 kupitia ukurasa wake wa Twitter, Ziito ameandika,“Nawapongeza CCM kwa ushindi  wa halali kabisa Jimbo la Muhambwe. Kila la heri kwa mbunge mpya.Tutakutana uchaguzi unaofuata tukiwa imara zaidi.

 

“Nampongeza msimamizi wa uchaguzi wa Muhambwe na OCD wa Kibondo kwa kufanya kazi kwa weledi,ninalaani matukio ya kuumiza watu yaliyotokea,”ameandika Zitto.

Leave A Reply