The House of Favourite Newspapers

Zitto Kabwe Akamatwa na Polisi Dar

0

MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa nyumbani kwake leo asubuhi na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Chang’ombe.

Jeshi la Polisi bado halijaeleza sababu ya kukamata, lakini Chama cha ACT Wazalendo, kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Yeremiah Kulwa Maganja  wamesema kwamba, sababu ya kukamatwa kwa Zitto Kabwe ni kutokana na mkutano wao wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika Kijichi mwishoni mwa juma.

ACT-Wazalendo imesema sababu za kukamatwa Zitto Kabwe ni hotuba aliyoitoa Kijichi wakati wa kuzindua Kampeni za Udiwani.

Aidha, ACT Wazalendo wameeleza kwamba, wanasheria wa Chama wanashughulikia kujua sababu za ukamatajwi huo Zitto ambaye pia ni kiongozi wa chama hicho.

LIVE: Rais Magufuli Azindua Kiwanda cha Victoria Moulders Igogo Mwanza

Leave A Reply