The House of Favourite Newspapers

Ndugai: Zitto Muongo Ananichafua, Lissu Tumempa Mil 250 za Matibabu – Video

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amesema kuanzia sasa ataanza kumjibu mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, kwa kuwa anaamini amepona na kwamba tayari ameshalipwa Sh 250 milioni kutoka bungeni kwa ajili ya matibabu yake aliyofanyiwa akiwa nje ya nchi.

 

Ndugai amesema hayo bungeni jijini Dodoma na kukanusha taarifa za kutomjali kifedha mbunge huyo huku akisema hadi sasa Bunge limeshamlipa Lissu kiasi cha Sh. milioni 250, kati ya hizo  mil. 207.8 ni stahiki zake na 43 ni mchango wa matibabu ya mbunge huyo aliyepigwa risasi Septemba 7, 2017.

 

 “Bunge limeshamlipa malipo mbalimbali Tundu Lissu kiasi cha Sh milioni 250 hadi sasa, namsubiri akanushe hili nilete mkeka,” alisema.

 

Lissu alishambuliwa jijini Dodoma ambapo alisafirishwa kwenda Kenya na hatimaye Ubelgiji kwa ajili ya matibabu.

 

Godbless E.J. Lema. (Twitter):

“Bunge halijawahi kumlipia Mh Lissu pesa kwa ajili ya matibabu, alichokisema Mh Spika Ndugai ni upotoshaji kwa jamii na Mungu. Chama kitatoa tamko juu ya hili. Spika akiweza kuthibitisha hili, Mimi nitajiuzulu Ubunge, mshahara wa Mbunge sio hisani ya Spika.”

 

Kuhusu Zitto na CAG, Ndugai amesema:

“Mwanzoni mwa mwaka huu, Zitto aliandika mitandaoni kuwa CAG alikuwa amefanya ukaguzi maalum Hazina, na kubaini wizi au ubadhirifu mkubwa wa Sh. Triliini 1.5 na ripoti yake kuiwasilisha ofisi za spika, na spika ameikalia. Ndugu yetu Zitto amekuwa muongo, haipendezi kwa mtu mzima, kama hiyo barua ya CAG anadai imeletwa kwangu na kipindi hicho wabunge wote tulikuwa likizo, yeye amejuaje? Anafanya kazi ofisi ya CAG?”

 

“Barua ya CAG niliipata tarehe 16 nikaipelema kwenye Kamati ya PAC. Hivi kweli ubadhirifu ya Sh. Tri 1.5 nikae kimya? Kama Sh. Milioni 300 za Escrow tulihangaika wote. Sasa hizi taarifa zingine ni kupakana matope ili spika aonekane mtu wa ajabu ajabu hivi. Mheshimiwa Rais alimuuliza CAG kama kuna upotevu wa Sh. Tri 1.5, sote tunakumbuka hapa tulikuwa tunatazama, CAG alikataa,” alisema Ndugai.

VIDEO: MSIKIE HAPA NDUGAI

Comments are closed.