The House of Favourite Newspapers

Zuchu Aandika Historia Dar Live, Shoo Yake ya Kibabe – Video

0

MSANII mwanadada anayekimbiza bongo kwa sasa kutoka Lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz, Zuchu ameandika historia mpya baada ya kupiga bonge la shoo katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam ikiwa ni shoo yake ya kwanza tangu atambulishwe kwenye game ya muziki.

Kabla ya Zuchu kupanda jukwaani, wasanii mbalimbali walitangulia kupanda jukwaani na kupiga shoo zao za kibabe akiwemo mama yake mzazi, Malkia wa Mipasho, Khadija Omary Kopa na kundi lake la Ogopa Kopa.

Zuchu alipanda Jukwaani majira ya saa 8:00 usiku na kushangiliwa na umati mkubwa wa mashabiki waliojaa uwanjani hapo wakimsubiri kwa hamu usiku huu wa kuamkia Jumamosi, Mei 15, 2021.

Hii imekuwa ni show ya kibabe iliyovuta maelfu ya mashabiki wa muziki kumshuhudia Zuchu akiimba hits songs zake zote ikiwemo Sukari na Number One pamoja na nyingine katika usiku wa Shangwe za Eid na Zuchu.

Wasanii wengine waliopiga shoo ni mkongwe wa Bongo Fleva, Juma Nature ambaye naye alisepa na kijiji kama kawaida yake.

Tazama mwenyewe hapa.

Leave A Reply