The House of Favourite Newspapers

Zuchu Amtisha Yemi Alade, Atinga Nne Bora Wasanii Wenye Wafuasi Wengi YouTube

0
                     Malkia mpya wa Bongo Fleva anayeitumikia Lebo ya WCB Zuchu

ZUHURA au Zuchu ni malkia mpya wa Bongo Fleva anayeitumikia Lebo ya WCB ambaye ameweka rekodi nyingine baada ya kutinga kwenye nne bora ya wanamuziki wa kike kutoka barani Afrika wenye ufuasi mkubwa kwenye mtandao wa YouTube akimtisha Yemi Alade wa Nigeria.

Zuchu ambaye ametajwa kama mwanamuziki anayekua kwa kasi ya ajabu kimuziki tangu kutambulishwa kwenye lebo ya WCB mwaka 2020, amefikisha wafuasi milioni 1.9 kwenye YouTube hivyo kuwa mwanamuziki wa kike wa nne barani Afrika kupata idadi hiyo ya wafuasi.

Namba moja inashikiliwa na Sherine kutoka Misri ambaye amejizolea wafuasi zaidi ya milioni 4.22, anafuatiwa na Zina Doudia kutoka Morocco akiwa na wafuasi milioni 3.04 kisha Malkia wa Afrobeats kutoka Nigeria, Yemi Alade akiwa namba tatu na wafuasi milioni 1.96

Sasa Zuchu kutoka Tanzania ana wafuasi zaidi ya milioni 1.9 akitazamia kumpiku Yemi Alade muda wowote.

Leave A Reply