The House of Favourite Newspapers

Zuchu Apambania Kombe Kwa Diamond, Aoneshana Mahaba Mazito Bila Woga

0
Malkia mpya wa muziki nchini Tanzania, Zuchu akidendeka na Diamond ambaye ni bosi wa Lebo ya WCB.

 

Zuhura Othman wengi wanamjua kama Zuchu; ni malkia mpya wa muziki nchini Tanzania ambaye ameapa kupambania kombe kwa bosi wake, Diamond Platnumz.

 

Zuchu na Diamond ambaye ni bosi wa Lebo ya WCB inayomsimamia mrembo huyo, kwa muda mrefu sasa inasemekana ni wapenzi.

 

Zuchu ndiye amekuwa akideka zaidi kwa Diamond au Mondi huku wenyewe wakinunuliana mijizawadi kedekede na kuambatana sehemu nyingi wanazokuwa.

 

Kama utakumbuka, hivi karibuni Zuchu alikuwa na shoo nchini Nigeria ambapo akiwa huko alifanya shoo kali iliyomfanya Diamond amtumie zawadi hukohuko.

 

Lakini kama hiyo haitoshi, Zuchu alimshtukiza Diamond baada ya kutokea Nigeria na kutua moja kwa moja jijini Mwanza ambako jamaa huyo alikuwa na shoo ya kibabe.

 

Wakiwa jukwaani, ndipo Zuchu na Diamond wakaoneshana mahaba mazito bila woga wowote huku wakishikana maeneo hatarishi bila kujali macho ya watu.

 

Zuchu amekuwa akishindwa kuficha kabisa kuficha penzi lake kwa Diamond na jinsi ambavyo jamaa huyo ameweza kumnogesha.

Hata hivyo, Zuchu amekuwa akisemwa mno kwenye mitandao ya kijamii kuwa haendani na Diamond, hanogi wala kudamshi anapokuwa na jamaa huyo.

 

Wengine wameenda mbali na kusema Zuchu haendani na jamaa huyo ambaye ana uwezo wa kuwa na pisi kali yeyote kuliko yeye.

 

Katikati ya mjadala huyo, Zuchu ameibuka na kulitetea penzi lake hilo akisema; “Msione mtu anamng’ang’ani mtu, kuna vitu havielezeki…”

 

Hata hivyo, miezi sita baada ya penzi hilo, baadhi ya watu wanakiri kwamba Zuchu amembadilisha kwa kiasi kikubwa Diamond huku msingi mkubwa ukiwa ni kumsisitiza juu ya suala kumuogopa na kumcha Mungu kwa kumkumbusha sana suala la ibada.

 

Watu wa karibu wanasema Zuchu ameshika mno dini yake ya Kiislam hiyo mara zote humkumbusha Diamond kwenda kusali pale tu muda wa kuswali unapowadia.

Stori; Khadija Bakari, Dar

Leave A Reply