The House of Favourite Newspapers

Zuchu Asifia Mpenzi Wake… Kisa Kipo Hapa

0
MALKIA mwingine wa Bongo Fleva, Zuhura Othman au Zuchu amemsifia mpenzi wake baada ya kumnunulia zawadi ambayo alikuwa anaitamani mno.
Zuchu amesambaza video iliyoambatana na sauti yake, akieleza furaha yake baada ya kupokea zawadi ya mdoli aliokuwa ameagiza kutoka kwa mpenzi wake.
Kwenye video hiyo, inaonesha mdoli aliyeletewa Zuchu na mpenzi wake huku akionekana mwenye bashasha isiyokuwa na kifani.
Zuchu anamshukuru mpenzi wake ambaye muda wote amekuwa akificha jina na sura kwa zawadi aliyompatia.
Kwa mujibu wa Zuchu, alitaka mpenzi wake amnunulie mdoli mkubwa, lakini alichokuwa hana uhakika nacho ni kuwa hakutarajia kununuliwa mdoli mkubwa kiasi hicho.
Baadhi ya wafuasi wake walimemcharukia Zuchu wakimtaka aseme ni mpenzi gani aliyemletea zawadi hiyo.
Hata hivyo, hivi karibuni, Zuchu alitangaza kuwa yuko singo na hana haraka ya kujihusha na mapenzi; ilikuwa
ni baada ya kuibuka kwa uvumi kwamba yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na bosi wake, Diamond Platnumz

Leave A Reply