The House of Favourite Newspapers

Zuchu Atimiza Ndoto Ya Mama’ke (Picha +Video)

0

Nani kama mama? Kama Mwenyezi Mungu akikujaalia chochote kwa nini usimjali mama yako kama alivyofanya sexy lady wa Bongo Fleva?

Basi bana, mchongo upo hivi; Staa mpya wa kike wa Bongo Fleva anayetumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman ‘Zuchu’ Juni 16, 2021 ametimiza ndoto ya kitambo ya mama yake, kumiliki gari aina ya Toyota Toyota Alphard lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 za Kitanzania kama ukilikuta kwenye yadi.

Zuchu mwenyewe ameandika; “Hatimaye nimemnunulia mama yangu gari analolipenda zaidi.

“Video ya kwanza ilikuwa mwezi uliopita, nilimuuliza anapenda gari aina gani?

“Nina furaha mno, miezi 12 iliyopita sikuwa na uwezo hata wa kumlipia nauli Mama’ngu. Allah akuweke uzidi kula matunda yako, mama unastahili zaidi ya hili mama’ngu…@officialkhadijakopa.

“Mwenyezi MunguaAtujaalie sote uwezo wa kuwatunza wazazi wetu Amen. I love you mummy.”

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply