The House of Favourite Newspapers

Zuchu Balozi Mpya Bidhaa za Tridea Cosmetics

0
Zuchu alivyowasili Tridea Cosmetics leo.

Kampuni ya vipodozi ya Tridea Cosmetics, inayofuraha kutangaza kuingia makubaliano na msanii Zuhura Othman ‘Zuchu’, kuwa balozi wa bidhaa zake.

Zuchu ambaye ni msanii wa muziki wa bongo fleva katika lebo ya WCB, atakuwa balozi wa bidhaa za Tridea akihusika kwenye matangazo ya TV, magazeti na mitandao ya kijamii.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tridea Cosmetics, Grace Luswaga akimtangaza Zuchu kuwa balozi wa bidhaa zao.

“Zuchu ni msanii wa kike anayekubalika kwa sasa na atakuwa balozi mzuri kwa wengine kupitia bidhaa zetu ikiwemo kuwasaidia wanawake kutumia na kujisikia vizuri.

“Tumeamua kufanya naye kazi baada ya kuona kazi zake zinakubalika na atakuwa balozi mzuri kwa wengine,” alisema Mtendaji Mkuu wa Tridea Cosmetics, Grace Luswaga.

Zuchu akizungumza kwenye hafla hiyo baada ya kupewa ubalozi huo.

“Bidhaa za Tridea kwa wanawake zinasaidia kuwaweka kwenye mwonekano mzuri na kujisikia huru kila wakati,” alisema.

Akizungumzia hilo, Zuchu alisema kuwa amefurahia kuingia mkataba na Tridea Cosmetics na huo utakua ushindi wa wanawake wote na kina mama wa Tanzania nzima.

Akikagua baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo.

“Ninafurahia kuingia mkataba na Tridea Cosmetics na kwani nitakua balozi mzuri kwa wanake wenzangu na kina dada, mama yangu pia anatumia bidhaa hizi na mimi tangu nikiwa mdogo nimekuwa nikizitumia,” alisema Zuchu.

Zuchu akizungumza jambo na Meneja wa Mauzo kampuni hiyo, James Fernandes kulia ni meneja wa Zuchu aliyejitambulisha kwa jina la Doris.

Zuchu ni msanii aliyetoka kwenye familia ya muziki ambapo ameshashirikishwa kwenye wimbo wa Mauzauza na mama yake Khadija Kopa, pia Cheche ya Diamond Platnumz.

Zuchu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tridea, Grace Luswaga wakielekea kwenye uzalishaji wa bidhaa hizo.

Zuchu kwa sasa anafanya vizuri katika muziki wa bongo fleva na kuendelea kuwateka mashabiki kila kona ikiwemo mitandao ya kijamii.  HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL 

Leave A Reply