The House of Favourite Newspapers

Familia Iliyoteketea kwa Moto… Chanzo Chajulikana

0

moto (11)     Tatu Issa na mjukuu wake, Catherine Stewart enzi za uhai wao.

Stori: Waandishi Wetu, Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Bado inauma sana! Kufuatia moto kuteketeza familia ya Eliakunda Mbwambo yenye watu watatu, mke, Tatu Issa (50), binti, Rehema Mbwambo (27) na mwanaye wa kwanza, Catherine Stewart (6) chanzo cha ukatili huo kimejulikana.

Tukio hilo lilijiri Mei 15, mwaka huu, nyumbani kwa familia hiyo, Migombani, Minazi Mirefu, Kiwalani jijini Dar es Salaam na kuandikwa na gazeti hii la Mei 21, mwaka huu na kichwa cha habari; Moto wa ajabu wateketeza mjamzito, mtoto na bibi.

moto (8)

Marehemu, Rehema Mbwambo

Hata hivyo, Eliakunda mwenyewe ambaye alinusurika na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) naye alifariki dunia Mei 23, mwaka huu kufuatia sehemu kubwa ya mwili wake kuungua.

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kabisa, aliyelengwa kutolewa uhai katika tukio hilo ni Rehema ambapo habari zinadai kuwa, uhasama wake na mwanaume mmoja (hakutajwa jina) ndiyo chanzo.

“Rehema aliwahi kuniambia amekuwa akitongozwa na mwanaume mmoja na alishakula pesa zake sana lakini hakuwa tayari kuwa na uhusiano naye.

“Akaniambia hali hiyo ilikuwa ikimfanya jamaa kumbembeleza kila wakati lakini yeye alikuwa hataki licha ya kwamba alikuwa akipokea pesa zake.

moto (4)

Nyumba ilivyoteketea kwa moto

“Sasa siku moja yule jamaa alipata habari kwamba, Rehema ana ujauzito wa mwanaume mwingine maana baba wa mtoto wake, Catherine walishatengana, ikamuuma sana!

IMG-20160521-WA0010 Majeneza yenye miili ya marehemu

“Kwa hiyo huenda kwa hasira huyo mwanaume ambaye mimi simjui, usiku huo wa Jumapiili ndiyo alinunua petroli na kwenda kuimwagia nyumba hiyo na kuichoma moto mpaka watu wanne  kupoteza maisha.

“Inauma sana maana hata moto wenyewe ulikuwa unatoa harufu ya petroli! Lakini Rehema mwenyewe alikuwa akisema alishindwa kuwa na uhusiano na mwanaume huyo kwa vile alishakuwa na mtu mwingine na ndiye aliyempa ujauzito,” kilidai chanzo hicho.

moto (5)Awali baadhi ya majirani walisema kuwa, huenda tukio hilo lilikuwa na mambo ya kishirikina kwani nyumba hiyo haina umeme na moto ulianzia mlangoni lakini chumbani haukufika japokuwa Eliakunda alilala huko na aliungua moto.

IMG-20160522-WA0001Waomboezaji siku ya mazishi

Kwa upande wa jirani aliyejitambulisha kwa jina la mama Conso alisema wakati wa tukio hilo walisikia sauti zikiomba msaada kwamba wanakufa hivyo aliamka na kukimbilia huko na kukuta moto ukiwa unawaka huku majirani wengine wakiendelea kupiga kelele za kuomba msaada.

moto (6)

“Ilikuwa ni saa nne usiku, nilisikia kelele zikiita mama Conso tunakufa tuokoe ndipo tukatoka na kukuta moto, tukaanza kufanya jitihada za kuuzima na kuwapigia fire ambao nao walikuja ambapo waliwaokoa wakiwa wameshakata kauli, walikwenda kufia hospitali,” alisema mama Conso.

Diwani wa kata hiyo ya Minazi Mirefu, Kassimu Mshamu akizungumza msibani hapo alisema amesikitishwa sana na tukio hilo kwani haijawahi kutokea,  hivyo kupoteza watu wanne wa familia ni majonzi makubwa yasiyokuwa na mfano.

Moto Ilala (9)

Akizungumza na gazeti hili, baba wa Catherine alisema ameumizwa sana na vifo hivyo kwani aliyekuwa anamuona ana nafuu ya kupona ni mwanaye lakini alifariki dunia na kumuachia majonzi.

“Mimi na mama Catherine tuliachana miezi sita iliyopita hivyo baada ya kupata taarifa hizi nilifika na kwenda kuwahudumia hospitalini lakini Mungu akawapenda zaidi. Nakumbuka mwanangu alivyokuwa akilia na kuomba apelekwe hospitali, anaumia huku akimuulizia mama yake na bibi.

moto (1)Hudhuni ikitanda

“Mimi nilibaki namuuguza mzee Eliapenda hospitali na alipata nafasi ya kuzungumza  akasema ule moto ulisababishwa na mtu lakini hakumtaja jina kwani alikata kauli,” alisema baba Catherine.

Imeelezwa msibani hapo kuwa polisi walikuwa wakijipanga kwa ajili ya kumsaka mhusika wa mauaji hayo. Miili ya watu hao wanne ilizikwa Jumatano iliyopita kwenye Makaburi ya Kiwalani, Dar.

Imeandikwa na Imelda Mtema, Mayasa Mariwata na Gladness Mallya.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply