The House of Favourite Newspapers

Kigogo wa Sukari: Magufuli ametunyoosha

0

MagufuliiRais John Magufuli

Na Ojuku Abraham, RISASI MCHANGANYIKO

DAR ES SALAAM: Mfanyabiashara mmoja mkubwa, ambaye hivi karibuni alikutwa na tani nyingi za sukari katika ghala lake (jina lake linahifadhiwa) amekiri kuwa utawala wa Rais John Magufuli umewanyoosha kwa vile hataki mchezo kazini.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake hivi karibuni, pamoja na kutoa ufafanuzi wa jinsi anavyoifanya biashara hiyo kwa mujibu wa utaratibu, lakini pia alisema wafanyabiashara wamejikuta wakilazimika kufuata sheria na kuacha konakona kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Sukari

“Sukari iliyokutwa kwangu haikuwa na matatizo ndiyo maana hakuna hatua zilizochukuliwa kwa sababu ipo ‘clean’ (halali), lakini nikuambie ndugu yangu, Magufuli katunyoosha, katufanya tuufyate, maana sasa hivi hakuna konakona, zamani ungeweza kusema ngoja nifanye ujanja, lakini hakuna,” alisema bila kutoa ufafanuzi zaidi wa kauli hiyo, licha ya kuombwa kufanya hivyo.

Baada ya Rais Magufuli kupiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje, akidai baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu huagiza bidhaa hiyo ikikaribia kumalizika muda wake, uhaba mkubwa ulijitokeza, huku kukiwa na tetesi za bidhaa hiyo kufichwa makusudi ili kupandisha bei sokoni.

Kufuatia hali hiyo, rais aliagiza kukamatwa kwa wafanyabiashara wote watakaobainika kuificha sukari hiyo, hali iliyosababisha baadhi yao, wakiwemo Harun Zacharia, Haidary Mohamed, Mohamed Enterprises na wengineo kukutwa nayo kwenye maghala yao na hivyo kuhojiwa na vyombo vya dola.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply