The House of Favourite Newspapers

Nay; Sasa hebu shika adabu yako!

0

Nay (3) Na Ojuku Abraham

EMMANUEL Elibariki ndilo jina lake halisi, lakini amejipatia umaarufu mkubwa kwa jina la Nay wa Mitego katika Muziki wa Bongo Fleva. Unapozungumzia marapa vijana waliochipukia baada ya wakongwe kina Sugu, Prof Jay, Fid Q, AY, FA na wenzao wa kizazi hicho, huwezi kumuweka kando dogo huyu.

Ninasikiliza mara nyingi kazi zake na mojawapo iliyonikaa ni ile aliyofanya kolabo na Diamond ya Muziki Gani. Ukiisikiliza ile ngoma, ndipo unatambua jinsi gani rap na uimbaji unaweza kuleta kitu tofauti ukichanganywa. Lakini zaidi kilichonivutia, ni ule ukweli wa mipasho waliyokuwa wakibadilishana na Diamond.

Nay (9)Sauti nene

Moja ya vitu vikubwa vinavyombeba Nay ni sauti yake nene na jinsi anavyotambaa kwenye midundo ya muziki wake, ni jambo lingine linalokufanya uvutiwe naye. Ni mtu anayekufanya usione pengo linaloonekana kuwepo la kukosekana kwa Chid Benz katika ubora uliotukuka.

Ukweli wa Hip Hop

Ninafahamu, Hip Hop ni aina ya sanaa ya tambo, yenye kuakisi ukweli wa maisha ya jamii. Ndiyo maana nchini Marekani, wengi waliofanya Hip Hop ni kama wanaharakati wa kutetea haki ya watu weusi, ambayo walikuwa wakiielezea kwenye nyimbo na video zao, kama jinsi wanavyobaguliwa, kuteswa au kudhalilishwa na weupe, achilia mbali pia kuwa waliitumia kutamba, kuonesha ufahari wao katika mambo mbalimbali.

Marapa wa Bongo niliowataja pale mwanzo, walifanya hivyo pia na kujizolea umaarufu mkubwa, kwa kuwa walizungumza mambo yenye kuakisi maisha halisi ya jamii yao.

Anapokosea Nay

Ukichunguza sana nyimbo za Nay, unagundua kuwa licha ya kutembea kwenye Hip Hop kwa maana ya tambo, lakini ana ukweli uliopitiliza ambao maadili ya jamii iliyomkuza yanamkataza.

Katika ngoma yake ya Nasema Nao, kuna mistari inayowa-dhalilisha akina dada wa Bongo Muvi pia katika Ngoma ya Shika Adabu Yako, pia ametoa kashfa za kutosha tu kwa wenzake hadi wengine kuwadhalilisha.

Na mara zote hizo, wadau wakiwemo Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), wamekuwa wakimpigia kelele kiasi cha kufikia hata ngoma yake ya Shika Adamu Yako kufungiwa. Lakini kana kwamba haitoshi, hivi karibuni msanii huyu ameachia ngoma nyingine, Pale Kati Patamu, dah! Haifai.

Nimetazama ‘clip’ ndogo ya video ya ngoma hiyo, kwa kweli haufai. Huu unawafaa zaidi akina P Diddy ambao hata asili yao hawaijui.

Ushauri kwa Nay

Nimshauri Nay, yeye bado bwana mdogo sana kwenye huu muziki, ana kipaji kizuri tu na tena nje ya jukwaa, ana nidhamu ya kutosha. Aaachane na aina hii ya Hip Hop, itamuondoa sokoni na wanaokashifiwa au kudhalilishwa na mashairi yake wanaweza kumpeleka jela.

Maisha ya usela yana muda wake na unapofikia hatua ya kumiliki hela za kutosha, jina kubwa na hadhi, unahitaji nini tena zaidi ya heshima? Huu ni wakati wa Basata kuonesha makucha, siyo tu kumsh-ikisha adabu Nay, bali pia studio zinazote-ngeneza nyimbo na video zake!

Leave A Reply