The House of Favourite Newspapers

Sabby Angel, Bob Junior wadaiwa kurudiana

0

sabbyangel150115Sabrina Omary ‘Sabby Angel’

Stori: Boniphace Ngumije

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, anayesumbua na Ngoma ya Inahusu, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ anadaiwa kurudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake siku za nyuma, Mbongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ waliyeachana na kila mmoja kushika hamsini zake.

bob_junior_sharobaro2Bob Junior

Kwa mujibu wa chanzo, Sabby na Bob Junior walionekana kungandana kimahaba pande za Sea Breez, Mbezi Beach jijini Dar walipokuwa kwenye shoo iliyowakutanisha wasanii wa Bongo Fleva wakiwemo, Mesen Selekta, Khadija Kopa, Pam D na wengine wengi.

Sabrina Omary na bob juniour“Siku hiyo, Sabby na Bobby Junior walikuwa wamegandana kuliko kawaida kuanzia wanaingia mpaka mwisho, watakuwa wamerudiana wale lakini wanaficha tu,” kilisema chanzo hicho.

BMM ilimvutia waya Sabby ili aweze kufungukia tetesi hizo, akafunguka:

“Ni kweli niliwahi kuwa na Bob, lakini tangu tuachane kila mtu alishika hamsini zake na hatujawahi kuwaza kurudiana, kuwa pamoja kwa sasa ni kampani ya kikazi tu,” alimaliza Sabby huku Bob Junior simu yake ikiita bila kupokelewa.

Leave A Reply