The House of Favourite Newspapers

Vanessa Mdee, Rotimi na Kisa cha P Funk na Kajala

0

V MONEY, mtoto wa Arusha ni moja ya wasanii wanaopiga sana michongo ya nje na waliotengeneza bonge la connection katika muziki wake, ni rasmi sasa kaachana na Jux.

 

Jux na Vanessa walikuwa na mapenzi fulani ya kideoni. Jux mwanaume mtanashati mwenye kuvutia mademu kibao na Vanessa mwanamke mrembo, mjanja, anayejituma ila mwenye kipaji maridhawa cha muziki huku pia akiwa sumaku ya wanaume kadhaa.

 

Mapenzi yao yalikuwa na msisimko fulani wa kipekee. Kwanza ilivyojulikana kama wana-date, ilionekana kama Vanessa anatumia nyota ya Jux.

 

Ila kutokana na haso na michongo kibao ya Vanessa kutusua, ghafla akaonekana yeye ni maarufu zaidi kuliko Jux. Sasa ikaonekana Jux ndiye anasafiria nyota ya bimdada.

Mapenzi yao yalijaa drama za kila namna. Mara unasikia wameachana, mara wamerudiana katika majukwaa ya Fiesta.

 

Ila kila mmoja aliyewaona pamoja, alikiri walipendezana na safari yao ya kimapenzi pengine ingefika mbali zaidi. Bahati mbaya waliotabiri hivyo wamepotoka kama alivyopotoka aliyesema Mh. Edward Lowassa angekuwa Rais wa Tanzania mwakani 2015.

 

Jux na Vanessa kwa sasa kila mmoja ana mchongo wake. Jux kazama kwa Mzungu, Vanessa kaibuka na Mnigeria, anaitwa Rotimi. Ni jamaa fulani hivi mtanashati mwenye pua kama Jux.

Akifanya mahojiano na mtandao fulani hivi, Vanessa anasema anajihisi mpya kuwa na Rotimi katika mapenzi.

 

Anasema ni mwanaume wa kipekee, mwenye kujua kubembeleza na anahisi kachelewa kumpata. Ukisoma kauli zake juu ya mstari, maana yake ni kuwa Vanessa katika kipindi kifupi ana-enjoy zaidi mapenzi na Rotimi kuliko kipindi chote cha maisha yake alipokuwa na Jux.

 

Mapenzi bwana! Huwa yanachipua na kutoa harufu nzuri kama ua waridi ila yakioza hunuka kuliko mzoga wa mbwa kibonge.

 

V Money akatiririka zaidi na kusema alivyomuona Rotimi ndani ya siku mbili tu, alijua jamaa anafaa kuwa mumewe wa maisha.

Macho ya Vanessa yalimskani jamaa ndani ya siku mbili na kutoa majibu kuwa kama wakiwa pamoja, basi watadumu milele daima. Acha kabisa.

Nilimsikia Vanessa akisema hivi, nakumbuka kisa cha mtayarishaji wa muziki; P Funk Majani na Kajala Masanja.

 

Baada ya kudumu na Kajala kwa takriban miaka nane, P Funk akaachana na mrembo huyo wa Kisukuma mwenye rangi tamu nyeusi na shepu maridhawa ya kibantu yenye kufurahisha na kutesa wanaume wengi.

 

Kwa mujibu wa P Funk, baada ya kuachana na Kajala akajikuta akikumbwa na ‘stress’ hata zikamfanya ashindwe kutengeneza muziki kwa miaka miwili mfululizo.

 

Achana na kitu mapenzi. Stress zake zinaweza kukufanya ukatoka Sinza kwenda Posta kutafuta gari ya kurudi Sinza.

Kila nikifikiria kisa hiki namfikiria Vanessa Mdee. Ndani ya siku mbili ana amini Rotimi ni mume wake wa maisha. Bidada anajua athari ya kuwa katika mahusiano ya mzuka kiasi hiki?

 

Je, ni kweli anayosema kuhusu Jux ama anaamua kusema ili aonekane yuko sehemu salama zaidi ila ndani ya moyo wake anawaka moto wa kumkosa African Boy Jux?

Ni kweli kuna mapenzi yanayozaliwa kwa mwana mitindo Rotimi na Vanessa. Ila ni ngapi? Kati ya mahusiano hamsini yaliyodumu, ni mahusiano mawili tu ndio yametokana na mtindo wa love at the first sight.

 

P Funk Majani mtayarishaji mwenye kipaji na ubunifu mkubwa, alishindwa kufanya maajabu studio kwa miaka miwili kisa mapenzi.

 

Vanessa nini kimemfanya afikirie mapenzi kuwa ni kitu simple tu kama kukata mauno jukwaani?

Mapenzi yalimfanya Ray C kuingia katika uraibu wa madawa ya kulevya kwa sababu ya uhusiano wake na Lord Eyes. Kwa mujibu wa Ray C, wao walikuwa wakivuta tu ganja ila jamaa akawa anachanganya na ‘unga’.

 

Kutokana na kuzama penzini hata kushindwa kujitambua, akajikuta naye akianza kubugia madawa ya kulevya na hatimaye akadata hata kupoteza ramani ya muziki wake.

 

Kazi ya muziki inahitaji mazingatio na utulivu wa kihisia. Ni watu wachache sana wenye akili na fikra za kipiganaji ndio wanaweza kugeuza matatizo ya changamoto zao katika mahusiano kuwa nyimbo nzuri za kufurahisha.

 

Watu kama Barnaba na Diamond Platnumz, wamethibitisha kuwa matatizo yao ya kimapenzi yanaweza kuwa muziki mzuri katika masikio yetu na hisia zetu. Ila wengi wamechemsha.

 

Matatizo yao ya kimapenzi yamewakoroga hata kuwafanya wasijue wanafanya nini katika soko la muziki. V Money kwa Rotimi hali itakuwaje? Muda utazungumza!

Makala: RAMADHAN MASENGA

 

USIYOYAJUA KUHUSU MASHUJAA HAWA, RUGE, MUFURUKI, MENGI..

Leave A Reply