The House of Favourite Newspapers

Magufuli Azindua Kampeni za CCM kwa Kishindo – Video

0

Leo Agosti 29, Historia imekwenda kuandikwa upya katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, ambapo Wasanii zaidi ya 100 wata-perform kwenye Jukwaa la Uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

 

Maelfu ya wananchi wameanza kufurika uwanjani hapo kushuhudia uzinduzi huo wa kihistoria ambao utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni mgombea Urais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, Dkt. John Pombe Magufuli.

 

“Mungu anatupenda Watanzania, kazi ya Mungu haishindwi na ndiyo maana Mataifa mengine na hata mnapoangalia kwenye TV gonjwa hili bado lipo, niwashukuru sana viongozi wa Dini zote

 

“Hapa Jamhuri watu ni wengi sana, ndani na nje ya uwanja. Kutokana na hilo, Rais Magufuli amesema akichaguliwa kwa mara nyingine tena, jambo la kwanza atakalofanya kwa watu wa Dodoma ni kujenga uwanja mkubwa michezo.

 

“Mwaka 2015 Watanzania walitaka mabadiliko na Serikali ya awamu ya 5 imejitahidi kukata kiu zao, tumerudisha nidhamu Serikalini sasa hivi maofisini mnahudumiwa vizuri,tumedhibiti rushwa na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na waliofikishwa Mahakamani sio dagaa ni samaki wakubwa.

 

“Tumeboresha Sekta ya Madini na sasa Watanzania wananufaika akiwemo Bilionea Laizer, tulipoanza kuchukua hatua kwenye madini wengine walitubeza na mnawajua, wakasema tutafunguliwa kesi lakini sasa waliotubeza naamini wanaona aibu.

 

“Tangu nimekuwa Rais nimetembelea nchi 8 tu na zote za Afrika, najua wapo wanaosema mimi kutosafiri kumepunguza mahusiano yetu ya Kidiplomasia na Mataifa mengine hii sio kweli, bali tumeyaimarisha, tumefungua Balozi 8 nje na Mataifa mawili yamefungua Balozi zao hapa nchini.

 

“Kazi tulizozifanya ndizo zimetufanya tuje kuomba tena ridhaa ili tuziendeleze zisije kukwama. Tumenunua Ndege mpya 11, Nane zimefika na tatu zinatengenezwa. Katika Ilani mpya ya Uchaguzi tutanunua Ndege nyingine 5 mpya ndani ya miaka 5 ikiwemo ya mizigo.

 

“Walitutisha kwamba tutashtakiwa na kufikishwa mahakamani lakini sisi tukasema rasilimali hizi ni zetu, tumepewa na mwenyezi Mungu ili tunufaike nazo hivyo hatuwezi kumuogopa mtu yeyote. Naamini wale waliotubeza sasa wameaibika.

 

“Nawashukuru pia wasanii wetu ambao wametuburudisha na nataka niwaambie tukimaliza hotuba yangu tutakaa hapa ili leo tukeshe hapa…kwa sababu leo ni siku ya raha na mimi nitacheza kwelikweli. Tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu azidi kuliongoza na kulisimamia taifa letu ili hatimaye tukamilishe Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa amani na usalama na huku tukibaki wamoja. 

 

“Tuna mradi mkubwa wa FARKWA hapa Dodoma, mradi huu utatatua changamoto ya upatikanaji wa maji hapa Dodoma. Mwenye macho haambiwi tazama, ukitazama jana leo utaona tofauti, wataweza kweli ?, niwashukuru wanaccm na wananchi wa Dodoma kwa kujitokeza mahali hapa.

 

“Tumeimarisha usafiri wa anga kwa kununua ndege na kufufua shirika letu la ndege, awamu ya pili tutahakiksha tunanunua Ndege zingine tano, mbili kubwa za mizigo na zitakuwa zikienda moja kwa moja Ulaya. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, tumejipanga kuendelea kusimamia amani, umoja na mshikamano wa nchi yetu, amani tutailinda kwa nguvu zote.

 

“Niliamua kumchagua tena Samia Suluhu kuwa mgombea mwenza, sikutaka kuchagua mwingine wa kuja kujifunza, pia ni mzuri mnamuona mwenyewe alivyo mweupe ni mchapakazi na anajua kutekeleza malengo ya Watanzania bila kubagua vyama vyao.

 

“Tumepanga kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia Mil 5, mapato kutoka Dola Bil 2.6 hadi Dola Bil 6, tutapanua wigo wa vivutio vya Utalii, ikiwemo kukuza Utalii wa mikutano na uwindaji wa Wanyamapori na kuimarisha utalii wa fukwe.

 

“Ninawaomba ndugu zangu chama pekee chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo Watanzania ni CCM hivyo ndugu zangu ninaomba sana kura zenu, tupate kura zote, nimejitahidi kuyaeleza haya yote nikiwa nawaomba Oktoba 28 ni siku muhimu sana.

 

“Ni mambo mengi ambayo yanatakiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 5, ndio maana niliamua kumchagua tena kuwa mgombea mwenza Mama Samia, mama mchapa kazi, mama mwema, mama anayejua tunaelekea wapi…lakini pia mzuri nasema uongo ndugu zangu?,mnamuona alivyo mweupe.

 

“Mliyotutuma tumeyafanya vizuri, tupeni tena miaka 5 mingine, tuendelee, mazuri makubwa yanakuja, tutaendelea kusimamia amani, umoja na mshikamano na tutaulinda Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar, tutakuza uchumi, tutapunguza riba kwenye Mabenki.

 

“Tutahamasisha wataalamu wetu wanaoweza kutibu magonjwa kwa kutumia dawa za kienyeji ili watambuliwe kikamilifu badala ya kuwapuuza, watanzania walio katika mambo utafiti tutaongeza pesa kwa ajili ya kuwasomesha kwenye vyuo bora.

 

“Mwinyi amekuwa Waziri wa Ulinzi kwa miaka 10, kijana kama huyu anasimamia Mizinga, Vifaru na Mabomu na hajawahi hata siku moja kuamrisha kwenda kupiga watu ni kijana mwenye Moyo mzuri sana ana upendo.

 

“Nawaomba ndugu zangu chama pekee chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo ni CCM hivyo ndugu zangu ninaomba kura zenu, tupate kura zote, nimejitahidi kuyaeleza haya yote Oktoba 28 ni siku muhimu sana.

 

“Kipindi cha kampeni watakuja wengi na mtaelezwa mengi, wasikilizeni kwa makini ili siku ya kupiga kura mfanye maamuzi sahihi, uchaguzi huu utaamua tupate viongozi wa kutuletea maendeleo au tupate viongozi wenye ajenda zao binafsi.

 

“Tutatengeneza nguo hapa Tanzania ili tuzivae wao tuwapelekee mitumba, tutatenga fedha za kuziandaa Timu zetu za Taifa, mikakati ya kuwasaidia wasanii ikiwemo kuwapa mikopo itawekwa, michezo na sanaa tutibeba, tutazidi kudhibiti rushwa.

 

”Nawaomba kura wote, Wanachama wa CCM nawaomba kura, CHADEMA nawaomba kura, ACT nawaomba kura, CUF na Vyama vyote hadi wasio na Vyama naomba kura zenu. Tumeimarisha usimamizi wa rasilimali zetu ili lengo zitunufaishe sisi wenyewe, mtakumbuka suala la ule mchanga, aidha tumeanzisha vituo vya mauzo ya madini kila mkoa.

 

“Watu wengi wanadhani mimi kutosafiri sana nje ya nchi basi uhusiano wetu wa kidiplomasia umepungua, kitu ambacho si kweli. Balozi nane za Tanzania katika nchi 8 zimefunguliwa na mataifa mawili yamefungua Balozi zao mbili hapa nchini.

 

“Hadi sasa vijiji 9570 nchini vimeunganishwa na huduma ya umeme kutoka vijiji 2018 mwaka 2015 na hii ni utokana na serikali kupunguza gharama ya kuunganisha umeme kutoka Sh. 177,000 hadi kufikia shilingi elfu 27 tu.

“Mkandarasi wa ujenzi wa Uwanja mkubwa wa ndege wenye urefu wa Kilometa 3, ambapo ndege zitakuwa zinatoka hapa kwenda Ulaya bila kupitia sehemu yoyote, tunayafanya haya kwa kujua kuwa hapa ndio Makao Makuu ya nchi.
“Huduma ya upatikanaji wa mawasiliano imeboreshwa kutoka 79% hadi kufikia 94% hivi sasa, na kupelekea watumiaji wa simu kuongezeka na kufikia milioni 40. Aidha gharama za mawasiliano zimepungua, kutoka sh. 267 kwa dakika moja 267 hadi kufikia sh. 40 kwa dakika.
“Tulizielekeza halmashauri kutenga 10% ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu. Tumefanya mazuri kwa wananchi wetu, ndio maana tunawaomba tena wananchi watuchague ili tuendelee kuwafanyia mazuri.
“Kupitia uwekezaji kwenye elimu tumepata mafanikio makubwa, mathalani katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu ufaulu umeongezeka na kufikia 96.7% na katika shule 10 bora, 8 ni za Serikali. Shule za Serikali zilikuwa hazionekani kwenye 10 bora sasa zinaonekana.
“Tumeingia kwenye nchi zenye uchumi wa wakati mapema kabla ya melengo yetu kupitia dira ya taifa ya kufikia uchumi wa kati mwaka 2025, yote hii ni kudhihirisha kuwa kazi tumeifanya vizuri. Mliyotutuma kufanya katika kipindi cha miaka mitano tumefanya kwa kishindo kikubwa, naomba mtupe tena miaka mitano mingine.
“Nina imani kubwa, muda si mrefu tutaanza kuonja na kuona mavuno kwa kazi tulizozifanya na uwekezaji tulioufanya kwa kipindi cha miaka mitano. Tutaendelea kuimarisha mshikamano na umoja wetu, tutayalinda Mapinduzi matukufu ya Zanzibar lakini kubwa zaidi tutailinda amani yetu kwa nguvu zetu zote.
“Tutahamasisha ufugaji wa kisasa, na pia tutahamasisha ujenzi wa machinjio ya kisasa, pamoja na kuhamasisha mbinu bora za kisasa na matumizi ya mbegu bora. Tunataka tuichakate pamba hapa hapa nchini, ili tutengeneze nguo, tuzivae kisha tuwapelekee nje kama mitumba.
“Migodi midogo tumewamilikisha wazawa wa eneo hilo, lengo ni madini hayo yaweze kutunufaisha wenyewe. Madini haya Mungu ameyafanya kupatikana hapa kwetu ili yatunufaishe. Tumepanga kufanya upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara pamoja na bandari ya Kalema ili itunufaishe sisi na jirani zetu DR Congo. Aidha, tutanunua meli ya mizigo katika bandari ya Hindi na pia tutanunua meli tatu katika Ziwa Tanganyika.
“Tumepanga kufanya upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara pamoja na bandari ya Kalema ili itunufaishe sisi na jirani zetu DR Congo. Aidha, tutanunua meli ya mizigo katika bandari ya Hindi na pia tutanunua meli tatu katika Ziwa Tanganyika.
“Tutaendelea kutoa elimu bila malipo kama tulivyofanya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. “Tutaendelea kutekeleza miradi ya maji vijini na mijini ili kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji nchini, lengo likiwa kufikia mwaka 2025 upatikanaji wa maji nchini ufikie asilimia 90.
“Hapa Dodoma tumefanya mambo mengi lakini kubwa kuliko yote ni kuhamishia makao makuu ya Serikali hapa Dodoma ambayo ilikuwa ni ndoto na maono ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
“Uchaguzi huu ni muhimu sana, ni muhimu kwa sababu ni utaamua ni ama tuendelee na mageuzi tuliyoanziaha au turudi nyuma, uchaguzi huu utaamua kumchagua atakayekaa na nyinyi wakati wa shida au yule atakayewaacha na kuondoka zake na kuwasikiliza watu waliowatuma.
“Nawaomba sana siku ya Oktoba 28,2020 ni siku muhimu kwa Taifa letu na ni muhimu sana katika kuitengeneza Tanzania yetu. Sidhani kama hao wengine hata miradi tuliyoianzisha wataendeleza, na huenda mkiwachagua haya makao makuu wakayaondoa hapa Dodoma.
“Watanzania tuangalie mahali tulipotoka, hapa tulipo na mahali tunapoelekea. Tanzania ya sasa ni tofauti na ya Tanzania zamani. Ndio maana tunaomba mtupigie kura.
“Tusiridhike tu kwamba Magufuli ameshinda, bali twendeni tukapige kura. Twendeni tukipige kura ili mwaka huu likae fundisho kwa wapingaji wa maendeleo, likae fundisho kwa wanaotumika na mabeberu na likae fundisho kwa asiotakia Tanzania mema na amani yake,” amesema Magufuli.

Leave A Reply