The House of Favourite Newspapers

Bob Junior, Mrembo Wazua Gumzo

Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’

Na: GLADNESS MALLYA| RISASI JUMAMOSI| MIKITO NUSUNUSU

MSANII wa Bongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’  hivi karibuni alizua gumzo baada ya picha yake akiwa amepakatwa na mrembo kuvuja mitandaoni akidaiwa ndiye mpenzi wake wa sasa.

Bob Junior na Mrembo

Chanzo makini kiliiambia Mikito Nusunusu kuwa Bob Junior kwa sasa yupo kwenye penzi motomoto na mrembo huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja ambapo amekuwa akijiachia sehemu mbalimbali kama viwanja vya starehe na ufukweni kupunga upepo kama hiyo picha ilivyovuja kwani inaonyesha wakiwa ufukweni.

Baada ya picha hiyo iliyozua gumzo mtandaoni na kupata habari kwa chanzo, Mikito Nusunusu ilimtafuta Bob Junior ambaye alisema;

“Ni kweli hiyo picha tulikuwa tukijiachia ufukweni lakini huyo ni rafiki yangu wa kawaida tu siyo mpenzi wangu jamani na jina lake siwezi kukutajia kwa sasa.”

Comments are closed.