The House of Favourite Newspapers

Wewe si Mjamzito lakini Unakosa hedhi, Unaijua Sababu?

Na TABIBU WA AMANI| GAZETI LA AMANI| MAKALA AFYA

TATIZO la kukosa hedhi huku wakiwa si wajawazito ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo. Aidha, suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo.

Tatizo la kukosa hedhi au Amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa (secondary) maishani mwa mtu. Primary Amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti na mambo mengineyo.

Secondary Amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi (menopause) na wala hatumii njia zozote zile za uzazi wa mpango kama vile sindano au vidonge na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama

KWANZA MWANAMKE HUPATAJE HEDHI?

Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi ni lazima matezi yake ya Hypothalamus na Pituitary pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya kike Ovaries na mji wa mimba Uterus vifanye kazi zake sawasawa. Hypothalamus huchochea tezi la Pituitary kuzalisha Hormone chochezi ya Follicle au Follicle-Stimulating Hormone (FSH) pamoja na homoni ya Luteinizing (LH).

Hizi FSH na LH kwa pamoja huchochea Ovaries kuzalisha homoni za Estrogen pamoja na Progesterone. Kazi za Estrogen na Progesterone ni kusababisha mabadiliko katika ukuta wa Uterus yaani Endometrium ikiwepo kupata hedhi. Ili damu ya hedhi iweze kutoka nje, njia ya uzazi ya mwanamke haina budi kuwa huru yaani isiyo na matatizo yoyote yale.

AMENORRHEA HUSABABISHWA NA NINI?

Visababishi vya Amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke. Matatizo katika mfumo wa homoni: Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za Hypothalamus , Pituitary au Ovary.

Matatizo katika Hypothalamus: Matatizo katika Hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya Pituitary. Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya Ugonjwa huu  hujulikana kama Kallmann Syndrome.

Comments are closed.