The House of Favourite Newspapers

Ubalozi wa Kuwait Watatua Shida ya Maji Kwa Wanafunzi 5600 Dar

DAR ES SALAAM: Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem amezindua mradi wa visima vya maji kwa ajili ya kusaidia wanafunzi 5600 wa shule tatu za msingi Yombo jijini Dar es Salaam.
Mrisho Mpoto akiwa katika uzinduzi na balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem
“Tunashukuru sana kuwa hapa, ni furaha yetu mradi wetu umekamilika, tuna imani utasaidia wanafunzi wengi pamoja na kujenga mazingira mazuri kwa ajili ya kujisomea. Kwa hiyo kama ubalozi tumedhamilia kusaidia shule mbalimbali kama tulivyofanya hapa ili kuboresha elimu,” alisema balozi huyo.
Akiongea na wanafunzi hao pamoja na wadau waliojitokeza katika uzinduzi huo, Balozi alisema wameamua kusaidia shule hizo ili kujenga mazingira mazuri ya wanafunzi kupata elimu.
Aidha katika uzinduzi huo msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto alikuwa kivutio kikubwa kwa wanafunzi hao.
Kwa upande wa Mrisho Mpoto ambaye alizungumza kuhusu uzinduzi huyo, aliwataka wanafunzi kutumia vizuri mazingira hayo kwa manufaa yao.
“Kila mwanafunzi hapa ana ndoto yake, mimi ningependa mtumie vizuri haya mazingira, kwa sababu kuna wanafunzi wengine wanatamani mazingira haya ila wanayakosa, kwa hiyo ni vyema mkayatunza na kuyalinda ,” alisema Mpoto.

GABRIEL NG`OSHA/GPL

Comments are closed.