The House of Favourite Newspapers

Snura Afiwa na Mnenguaji Wake

Picha imetumika kumrejelea mcheza dansi wa Snura

Na HAMIDA HASSAN| GAZETI LA IJUMAA| STAR MIX

PIGO! Mwanamuziki Snura Mushi amepata majanga baada ya kuondokewa na mnenguaji wake aliyefahamika kwa jina la Dotto.

Taarifa zilizolifi kia gazeti hili zinaeleza kuwa, Dotto aliyekuwa mmoja wa madansa tegemezi wa Snura alifariki dunia hivi karibuni ikiwa ni siku chache baada ya kujifungua huku chanzo cha kifo chake kikiwa hakijafahamika.

Snura akizungumza waandishi wa habari

Akizungumzia msiba huo, Snura alisema Dotto ameondoka wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika lakini hana la kufanya zaidi ya kumshukuru Mungu.

Snura

“Dah! Nimeumia sana, siwezi kusimulia msiba wa Dotto kwani umenishitua sana, wanaomjua wanaelewa alivyokuwa akinipa sapoti kwenye shoo zangu ila hatuna la kufanya zaidi ya kumuombea kwa Mungu,” alisema Snura

Comments are closed.