The House of Favourite Newspapers

Fid q Aeleza Daz Baba Alivyokuwa Akimgeuka

Fareed Kubanda ‘Fid Q’

Na MWANDISHI WETU| GAZETI LA IJUMAA| SHOW BIZ

MKONGWE wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ kwa mara ya kwanza amefungukia ukaribu wake na mkongwe mwenzake, David Jacob ‘Daz Baba’ kuwa aliwahi kumgeuka kipindi wanatamba na Ngoma ya Umbo Namba 8.

David Jacob ‘Daz Baba’

Akizungumza na Showbiz, Fid Q anayebamba na Ngoma ya Kemosabe alisema, kipindi hicho Daz Baba alikuwa juu sana na alikuwa akipata shoo kutoka kwa mapromota bila kupumzika.

“Alikuwa akianzia Jumatatu ni mpaka Jumatatu anapiga shoo tu bila kupumzika na ndiyo maana naona alihiti sana kama Muziki ya Darassa. “Lakini sasa alikuwa akinigeuka, kwenye shoo alikuwa akimchukua mtu mwingine na kwenda kuimba naye kwa kukwepa kama nitakuwa naye tungegawana,” alisema Fid Q.

Comments are closed.